Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA ‘KUVIMBA KICHWA’…KABUNDA AFUNGUKA A-Z NAMNA NAMUNGO WANAVYOISHI NAYE…

KUHUSU ISHU YA ‘KUVIMBA KICHWA’…KABUNDA AFUNGUKA A-Z NAMNA NAMUNGO WANAVYOISHI NAYE…


Winga wa Namungo FC, Hassan Kabunda amesema licha ya kuaminiwa na kuingizwa kwenye kikosi cha kwanza kwenye timu hiyo, haimfanyi kuvimba kichwa bali kuendelea kuonyesha uwezo wake na kuipa mafanikio timu hiyo.

Kabunda aliyewahi kung’ara na huko nyuma na Mwadui na KMC, kwa sasa anaichezea Namungo aliyojiunga nayo msimu huu na ameweza kuwemo kikosi cha kuanza.

Kabunda alisema kuaminiwa kwake ni hatua kubwa, lakini haiwezi kumfanya kuvimba bali kuhakikisha anaisaidia timu.

Alisema Namungo ina wachezaji wenye ubora na kiwango hivyo ili kuonesha si bahati mbaya kupewa uhakika wa namba lazima afanye makubwa ili kulinda kiwango chake.

“Kocha ameona ninaweza kufiti kwenye mfumo wake, lazima nioneshe kile alichokiamini kwangu lakini kulinda kipaji changu siwezi kubweteka wachezaji ni wengi kikosini na kila mmoja ana ubora wake,” alisema Kabunda.

Kabunda mtoto wa zamani wa beki wa Yanga, Salum Kabunda alisema akili zao zote zipo kwenye mechi ijayo dhidi ya Ruvu Shooting, Septemba 11 katika Uwanja wa Majaliwa.

“Tunataka pointi tatu kwenye mechi hiyo ili kujiweka sehemu nzuri,” alisema na kuongeza:

“Wachezaji wote tuna ari na morali tukisubiri muda wa mechi hiyo, kwasababu kipindi cha maandalizi tulijifua sana na tunaamini tuko katika ubora wetu,” alisema nyota huyo ambaye ni mmoja kati ya wachezaji wenye kasi sana.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI DHIDI YA WABOTSWANA..KANOUTE, MKUDE WAPIGWA MARUFUKU SIMBA..CHANZO NI PASI