Home Azam FC BAADA YA KUONA ZORAN ALIVYOWAPELEKA PUTA SIMBA…AZAM FC WAAMUA KUMPA UKWELI HUU...

BAADA YA KUONA ZORAN ALIVYOWAPELEKA PUTA SIMBA…AZAM FC WAAMUA KUMPA UKWELI HUU MAPEMA KOCHA WAO MPYA…


KLABU ya Azam FC imesema  kocha wao mpya, Denis Lavagne atafanya kazi na makocha atakayewakuta kwa sababu wanataka kuendeleza walichonacho na si kuanza upya.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Thabit Zacharia ‘Zaka Zakazi’, alisema kocha huyo raia wa Ufaransa amekuja peke yake na wasaidizi wataendelea kuwa wale wale ambao walikiongoza kikosi baada ya kuondolewa kwa kocha Abdihamid Moallin.

“Anakuja yeye kwanza, anafanya kazi na anaowakuta, hayo mengine tutazungumza huko mbele, hatutaki kuanza tena upya, tunachotaka ni kuendeleza kile tulichonacho,” alisema Zaka Zakazi.

Kuhusu sifa za kocha huyo, Zakazi alisema ni kocha mkubwa mwenye mafanikio ndani ya nchi alizozifundisha pamoja na nje, mwenye kulifahamu soka la Kiafrika.

“Ni kocha mkubwa sana, kocha ambaye amefanikiwa ndani ya nchi alizokuwa anazifundisha na nje ana rekodi nzuri, lakini analijua soka la Afrika, amekuja tangu 2007 na hajaondoka Afrika, amefundisha kwenye kanda zote za Afrika, na hiyo siyo faida kwake tu, bali hata kwetu Azam FC.” alisema.

Mfaransa huyo amewahi kufundisha timu ya Taifa ya Cameroon 2011 hadi 2012, USM Alger na JS Kabylie zote za Algeria, Etoile Du Sahel (2013), Smouha ya Misri, Coton Sports (Cameroon) na Al Hilal ya Sudan.

Moja ya mafanikio yake makubwa ni kufika fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2008 akiwa na Coton Sport ya Cameroon na kupoteza dhidi ya Al Ahly ya Misri kwa jumla ya mabao 4-2.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YAO YA CAF KESHO...HAWA GEITA GOLD NAO HAWAKO KINYONGE AISEE....WAWATISHA WASUDAN...