Home Habari za michezo JOB AWACHANA MASTAA YANGA…”ACHENI DHARAU AISEE…ISHU NZIMA IKO HIVI

JOB AWACHANA MASTAA YANGA…”ACHENI DHARAU AISEE…ISHU NZIMA IKO HIVI

JOB AWACHANA MASTAA YANGA...

CLATOUS Chama wa Simba pamoja na baadhi ya mastaa wa Yanga wameichungulia droo ya mechi za robo fainali za michuano ya CAF inayozikutanisha timu hizo na wapinzani kutoka nchi za Morocco na Nigeria, kisha kila mmoja kula kiapo wakitamba kuwa safari heshima itawekwa Afrika.

Katika droo hiyo iliyofanyika juzi nchini Misri, Simba imepangwa kukutana na watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Wydad ya Morocco, wakati Yanga iliyopo Kombe la Shirikisho imepewa Rivers United ya Nigeria na mastaa wa timu hizo za Tanzania wameahidi makubwa katika hatua hiyo.

Timu hizo zimeweka rekodi ya kutinga kwa pamoja hatua hiyo na zitaanza mechi zao Yanga ikianzia ugenini na kumalizia nyumbani, tofauti na Simba itakayoanzia nyumbani na kumalizia ugenini kati ya Aprili 21-30 ili kukta tiketi ya kucheza nusu fainali zitakazopigwa mwezi ujao.

Wakizungumza na SOKA LA BONGO kwa nyakati tofauti mastaa wa timu hiyo, Simba ikio ngozwa na Chama, huku Yanga ikiwa ni nahodha msaidizi, Dickson Job, Farid Mussa na Jesus Moloko walisema wanatambua wamefikia hatua ngumu ya mtoano na wanatakiwa kushindana ili wasonge mbele.

Job kufika robo lilikuwa lengo la kwamba kwa Yanga na sasa wanatambua umuhimu wa kupata matokeo ya ushindi ili waweze kuvuka kizingiti hicho na kufika hatua nyingine na wanawaheshimu wapinzani wao hivyo wataingia kwa tahadhali.

“Tunakutana na timu ambayo tayari umepata naasi ya kucheza nayo na matokeo dhidi yao hayakuwa mazuri hivyo hatuwezi kufanya makosa kwa kurudia kile kilichotokea tunajiandaa kuhakikisha tunalipa kisasi bila kuzalau ubora wao,” alisema beki huyo wa kimataifa wa Taifa Stars na kuongeza;

“Ni timu nzuri lakini na sisi ni bora hivyo dakika 90 zitaamua ubora wetu na wao malengo yetu kama timu ni kuvuka hatua ya robo na kuingia nusu fainali hivyo tutapambana kuhakikisha hatupotezi nafasi tutakazozipata.”

Winga wa Jesus Moloko alisema malengo ya benchi la ufundi na wachezaji ni kutinga hatua ya nusu fainali hilo linawezekana kama tutawekeza nguvu na juhudi binafsi huko akisisitiza kuwa wapinzani wao Rivers United wanatimu nzuri lakini hilo haliwafanyi wakashindwa kufanya vizuri.

“Tutaingia kwa kuwaheshimu tunashukuru tunaanzia nyumbani kwao na kumalizia kwa Mkapa ni hatua nzuri kwetu kuhakikisha na sisi tunatumia vizuri nafasi ya ugenini na kumaliza nyumbani ambapo tutahitaji pointi zote tatu.”

Farid Mussa alisema wao kama wachezaji lengo lao ni moja watapambana kuhakikisha wanapata pointi zote sita nyumbani na ugenini na kujitengenezea nafasi ya kusonga hatua inayofuta huku akikiri kuwa hilo linawezekana wakiwekeza nguvu kwa pamoja na kuamini katika kutumia kila nafasi watakayoipata.

Kwa upande wa kiungo fundi wa Simba, Clatous Chama alisema baada ya ratiba kutoka wao kama wachezaji wamekaa pamoja na benchi la ufundi kuzungumzia ubora wa wapinzani wao na kufahamu umuhimu wa matokeo mazuri ili waweze kufikia lengo ambalo limekuwa likikwama mara kwa mara ndani ya misimu minne waliyoshiriki.

“Tunatambua ubora wa Wydad, ni timu ngumu na yenye uzoefu wa kutosha na mashindano haya wakiwa mabingwa watetezi lakini hilo halituzuii kufanya vizuri,” alisema Chama na kuongeza;

“Simba tuna timu nzuri pia tunataka kuvuka hatua hii na kufika nusu fainali hivyo kama wachezaji, tupo tayari kwa mapambano na kuhakikisha tunafuzu nusu fainali.”

SOMA NA HII  MCHAMBUZI;- MASTAA HAWA NDIO WAMEIANGUSHA YANGA JANA...WALISTAHILI KUFUNGWA 5..