Home Habari za Simba Leo STRAIKA HATARI BONGO ATOBOA SIRI ZA MASTAA UBELGJI…AMEZUNGUMZA HAYA

STRAIKA HATARI BONGO ATOBOA SIRI ZA MASTAA UBELGJI…AMEZUNGUMZA HAYA

STRAIKA HATARI BONGO ATOBOA SIRI ZA MASTAA UBELGJI...AMEZUNGUMZA HAYA

Anwary Jabir yupo Ubelgiji akiendelea kufanyiwa majaribio ya kucheza soka la kulipwa akitokea Kagera Sugar na mwenyewe amevunja ukimya kwa kusema kilichombeba hadi kupata dili hilo ni koneksheni nzuri aliyopata kwa wakala wake na kutaka wachezaji wengine nao kuchangamka.

Straika huyo wa zamani wa Dodoma Jiji, anajaribiwa na timu ya K.A.A. Gent baada ya wakala huyo, Denis Kidoto kulamba dili na Anwary alisema kama hata wenzake watakuwa na mawakala walioshapu itakuwa rahisi kupta dili za kucheza nje ya nchi na kuja kuwa msaada mkubwa kwa taifa kimataifa.

Anwary alifichua, wachezaji wengi wanatamani kupata dili za nje, lakini wanakwamba kwa kukosa kuwa na mawakala wa kuwasaidia kufikia malengo na kuwashauri ni wakati wa kuwapata watu wa aina hiyo kwa ajili ya ndoto wanazoishi.

“Kiukweli bila kuwa na wakala ingekuwa ngumu kwangu kupata nafasi hii, kwani ndiye alitafuta hilo dili na kufanya niwe hapa, kilichobakia ni kupambana kuhakikisha naonyesha kiwango cha kuwashawishi wanisajili,” alisema Anwary na kuongeza;

“Nimeambiwa wanakuja wachezaji wengi kufanya majaribio wengine wanatoka Ghana, Ivory Coast ushindani utakuwa mkubwa, lakini kila mtu atapambana kwa kadri awezavyo.”

Alipoulizwa kuhusiana na mazingira yamekuwa ya aina gani kwake? Alijibu ni mzuri hayawezi kumzuia kupambana ili kupata fursa kupambania nafasi ya kusajiliwa ndani ya kikosi hicho.

Jabir mwenye mabao matano Ligi Kuu alisema; “Sitaki tena. kuchezea nafasi hii, nakumbuka kipindi cha nyuma wakati Abdi Banda yupo Baroka ya Afrika Kusini aliwahi kunitafutia nafasi lakini

nilizingua kwani nilikuwa na akili za kitoto ila awamu hii napambana.”
Banda anayecheza Chippa United ya Afrika Kusini alikiri ni kweli aliwahi kumtafutia dili Jabir lakini alikuwa na mambo mengi yaliyokwamisha safari yake.

“Kuna vitu vilitokea dili likafeli, lakini walikuwa wanamhitaji ndani ya timu na walipenda kiwango chake, ila yote katika yote apambane huko alikokwenda kufanya majaribio, naamini atafanikiwa,” alisema.

SOMA NA HII  SIMBA IMESHAKUWA JANGA MO DEWJI AOGOPA KUFA KWA PRESHA