KUELEKEA MECHI NA RIVERS...YANGA YAFANYIWA FIGISU HII...CAF YATUMIKA KUKAMILISHA MPANGO
Habari za michezo

KUELEKEA MECHI NA RIVERS…YANGA YAFANYIWA FIGISU HII…CAF YATUMIKA KUKAMILISHA MPANGO HUO

Marce Ben Komba April 11, 2023 8:56 am

Klabu ya Rivers United wameomba mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Yanga upigwe katika uwanja wao wa nyumbani, Adokiye Amaesimaka.

Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limefanya ukaguzi wa uwanja huo baada ya kufanyiwa ukarabati na sasa wanasubiri majibu kutoka CAF.
Rivers United hawakutumia uwanja huo katika mechi zao za hatua ya makundi baada ya kuzuiwa na CAF ukiwa umekosa vigezo.

Mchezo wa mkondo wa kwanza kati ya Rivers United dhidi ya Yanga utapigwa Jumapili Aprili 23 huko Nigeria na marudiano kupigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Aprili 30.

Yanga imepania kupata ushindi wa jumla katika mechi zote mbili na kutinga nusu fainali.

YANGA YAIPASUA KICHWA SIMBA…YAFANYIWA FIGISU KUBADILISHIWA UWANJA YANGA KUSHIRIKI LIGI HII YA WAFALME KWA MBELEKO…TFF YAHUSIKA…ISHU NZIMA A-Z IKO HIVI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply