Home Habari za michezo YANGA:-“FEI TOTO ACHA UJEURI…HUWEZI KUSHINDANA NA KLABU…ISHU NZIMA IKO HIVI A-Z

YANGA:-“FEI TOTO ACHA UJEURI…HUWEZI KUSHINDANA NA KLABU…ISHU NZIMA IKO HIVI A-Z

FEISAL SALUM

Klabu ya Yanga imemtaka mchezaji wao, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ kuacha ujeuri na kuitunishia misuli klabu yake hiyo badala yake afuate taratibu ikiwemo kwenda klabuni hapo na kufanya makubaliano na uongozi ili aweze kuondoka kwa heri.

Hayo yamesemwa leo Jumatano, Aprili 12, 2023 na Mkurugenzi wa Sheria wa Klabu ya Yanga, Wakili Patrick Simon mara baada ya kesi hiyo kushindwa kusikilizwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF kufuatia klabu hiyo kupelekea mapingamizi baada ya Fei Toto kuomba kuvunja mkataba wake na Yanga.

“Yanga imekuja na hoja nne za mapingamizi ya kisheria ambapo kwa mujibu wa taratibu za kimahakama, pale ambapo kunakuwa na mapingamizi basi kesi inasimama kusikilizwa badala yake mapingamizi yale yanasikilizwa kwanza mpaka mwisho, kwa hiyo Kamati imetoa fursa kwa pande zote mbili kujiandaa ili kuja kujibu hayo mapingamizi, kwa hiyo kesi haijaendelea.

“Tangazo la Yanga la Machi 6, 2023 lilikuwa wazi kabisa kwamba kama Feisal anataka kuondoka aje Yanga tuongee aondoke, kama kuna timu inamhitaji waje tuzungumze tumpe mkono wa kwa heri, tunashangaa anachokuja kukitafuta hapa (TFF) na tushampa options zote. Sisi hatujamng’ang’ania mchezaji mpaka ionekane tunamnyanyasa, hata leo akija akija tunamalizana anaondoka.

“Anachokifanya ni kutunisha mabega tu, kama angetaka kulinda kipaji chake sisi hatujamfanya kitu chochote, hajafukuzwa na Yanga, yeye mwenyewe ameamua kufanya utoro kaondoka kambini, hata hizo huruma anazozitafuta kwenye umma, sisi hatujamfukuza na tumempa option zote za kuondoka.

“Kama kaka yake, namshauri Fei Toto apunguze ujeuri, yeye hawezi kuwa mkubwa kuliko klabu, kwa hiyo ajishushe, asipojishusha… Yanga ni klabu kubwa, ilikuwepo kabla hajazaliwa na itaendelea kuwepo hata asipokuwepo tena,” amesema Wakili Patrick.

Fei Toto leo Aprili 12 alifika mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji kujua hatma ya barua yake ya kuomba kuvunja mkataba na klabu ya Yanga.

Fei Toto aliongozana na wakili wake Fatma Karume ambaye baada ya kumaliza kusikilizwa leo amesema kuna vitu vya kisheria vinatakiwa kuwasilishwa Aprili 18 na 25 na Mei 4 ndipo rasmi shauri litasikilizwa tena.
Sehemu ya barua inayotajwa kuandikwa na Feisal Salum kwenda TFF akihitaji kuvunja mkataba na Yanga. Amesema amepitia manyanyaso Jangwani na anaomba akacheze kule anapothaminiwa.

SOMA NA HII  HAWA HAPA WACHEZAJI MAJERUHI WA SIMBA NA YANGA WALIOPONA...LIST KAMILI HII HAPA