Pamoja na Yanga kuonyesha jitihada za kumwongezea mshahara beki wake Dick Job kutoka Sh milioni 4 hadi 6 milioni, nyota huyo ameweka ngumu na anataka ifike Sh milioni 10 jambo linaloleta ugumu kwa mabosi wa Yanga kuendelea kumshawishi kusalia ndani ya kikosi hicho.
Mkataba wa Yanga na Dickson Job unatamatika mwishoni mwa msimu huu na kuna uwezekano akatafuta malisho mengine.
Meneja wa Dickson Job, George Job aliweka wazi hivi karibuni kuwa hawana haraka ya kusaini Mkataba mpya kwa sasa.