Habari za michezo
IMEVUJA!! MABOSI SIMBA WAMWAGA MANOTI…WAIFUNGIA KAZI YANGA
Marce Ben Komba
April 14, 2023
2:54 pm
Mabosi wa Simba wameamua kuifungia kazi Yanga inayonolewa na Kocha, Nasreddine Nabi kwani wamesema hawataki chochote zaidi ya ushindi katika Kariakoo Dabi, ambapo tayari wameandaa bonasi ya kutosha ya zaidi ya Sh 300 Milioni kwa wachezaji ili kufanikisha ushindi jumapili.
Katika mchezo huo, Simba wataingia wakiwa na hasira ya kufungwa mara mbili mfululizo walizokutana katika Ngao ya Jamii msimu huu na uliopita.
Taarifa zinasema mabosi hao wa Simba kitu pekee ambacho wanakitaka katika msimu huu ni kuifunga Yanga, hiyo ni baada ya kushindwa kuifunga kwa misimu miwili.
Mtoa taarifa huyo alisema kuwa mabosi hao wa Simba, wameweka nguvu hizo za kuwafunga Yanga kwa ajili ya kuwapa furaha mashabiki wao.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.