MMH HII SASA KUFURU...MABOSI WA SIMBA WAINGIA KAMBINI NA TIMU
Habari za michezo

MMH HII SASA KUFURU…MABOSI WA SIMBA WAINGIA KAMBINI NA TIMU

Marce Ben Komba April 14, 2023 3:11 pm

Katika kuhakikisha wanashinda mchezo wa Jumapili (April 16) dhidi ya Young Africans, baadhi ya viongozi Klabu ya Simba SC kutoka kamati mbalimbali wamehamishia shughuli zao kambini ili kujihakishia ushindi.

Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, Young Africans na Simba zilitika sare ya bao 1-1. Na sasa Young Africans kileleni mwa ligi ikiwa na alama 68 mbele ya Simba wenye alama 60 tu.

Taarifa kutoka Simba SC zimeeleza kuwa, tangu kikosi hicho kimeingia kambini huko Mbweni baadhi ya viongozi wamekuwa wakishinda huko na kutoka usiku mnene ili kuhakikisha wanawatia moyo na nguvu wachezaji wao.

“Kiukweli tangu tuingie kambini kuna baadhi ya viongozi wamekuwa hawaishi mazoezini na kambini nadhani lengo ni kuendelea kutoa hamasa kwa ajili ya mechi yetu ijayo ambayo kila kiongozi anatutaka tuifunge Yanga,” zimeeleza taarifa hizo

Kwa upande wa Meneja Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema:

“Ukubwa na umuhimu wa mchezo huu kwetu ni lazima tushikamane maana tunahitaji kuifunga Young Africans tu.”

“Hakuna kiongozi au Mwanasimba anayetaka kuwaona Young Africans wakitangaza ubingwa dhidi yetu, hivyo tumejipanga kuvuna ushindi bila kujali staili tutakayoitumia maana hatujawafunga muda na sasa heshima yetu pekee ni kuwapa kichapo.”

IMEVUJA!! MABOSI SIMBA WAMWAGA MANOTI…WAIFUNGIA KAZI YANGA KOCHA UGANDA “YANGA WATAWAPIGA RIVERS…AMEZUNGUMZA HAYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply