KWA MKAPA KUMEDODA...MECHI SIMBA NA YANGA MASHABIKI HAKUNA...ISHU NZIMA IKO HIVI
Habari za michezo

KWA MKAPA KUMEDODA…MECHI SIMBA NA YANGA MASHABIKI HAKUNA…ISHU NZIMA IKO HIVI

Marce Ben Komba April 16, 2023 2:59 pm

Zikiwa zimebaki saa Chache kuanza kwa mtanange wa Simba na Yanga hali inaonekana kupoa nje ya Uwanja wa Benjamin Mkapa tofauti na ilivyozoeleka kwenye derby zilizopita.

Mchezo huo unaozikutanisha timu vigogo za Tanzania zenye mashabiki wengi unatarajiwa kupigwa kuanzia saa 11:00 jioni lakini hadi sasa shamrashamra nje ya uwanja zimeonekana kuwa chache.

Pamoja na kupoa, lakini biashara nyingine ndogondogo zimeonekana kuendelea huku mashabiki wakiendelea kufika eneo la tukio japo kwa uchache.

Hali ya hewa ipo shwari hadi sasa na maofisa mbalimbali wa ulinzi wakiwemo Polisi wapo pia nje na ndani ya uwanja wakiendelea kuhakikisha amani na ustaarabu.

Aidha kuna baadhi ya maeneo yameonekana kuendelea kuuza tiketi za kuingia uwanjani huku kukiwa na misongamano kwa makundi.

MERIDIANBET WAZIDI KULITEKA SOKA LA BONGO…..WAFANYA KWELI KWA TIMU ZA WANAWAKE… KOCHA YANGA “SIMBA TUMEWAFUNGA TOKA MAZOEZINI…TUNATAKA POINTI 3 TU…AMEZUNGUMZA HAYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply