Vilabu vilivyokuwa vikimnyemelea aliyewahi kuwa mchezaji wa Simba SC, Louis Miquissone zimeamua kuachana naye baada ya kiwango chake kuporomoka hali ilisababisha hata waajiri wake, Al Ahly kumtema.
Tangu arejee kwao Msumbiji baada ya kuachana na klabu aliyokuwa akiitumikia kwa mkopo akitokea kwa mabingwa wa kihistoria Afrika, Al Ahly, Louis ameshuka sana kiwango chake na hii ilipelekea hata kocha wake wa timu ya taifa kumuanzisha benchi,
Taarifa kutoka kwao Msumbiji ni kwamba kwa sasa anafanya mazoezi na moja ya Taasisi kubwa nchini ya kulea vijana ili kuangalia msimu ujao atajiunga na klab gani,
Ligi ikiisha hakutakuwa na mapumziko marefu sana , itakuwa kazi kuanza kumshape upya mchezaji mpaka arejee kwenye kiwango chake, pia bahati,anaweza asirejee pia Alisema mwana habari wa Michezo huyo kutoka Afrika kusini,
Moja ya klabu iliyokuwa imeonyesha nia ya kuitaka saini ya Winga huyo ni Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, ambayo imeamua kurudisha mkwanja wake benki na kuanza mkakati wa kusaka mchezaji mwingine badala ya Miquissonewaliokuwa wakimmezea mate.