Home Habari za michezo GEOF LEA :- TIMU BORA (YANGA) ILIFUNGWA NA TIMU YA HAMASA (SIMBA)…HATA...

GEOF LEA :- TIMU BORA (YANGA) ILIFUNGWA NA TIMU YA HAMASA (SIMBA)…HATA LIVER WALIIOKOTA MAN U…

Habazi sa Simba na Yanga

Mchambuzi wa masuala ya Soka nchini kupitia kituo cha radio cha EFM, Geof Lea amekiri kuwa ni kweli timu ya Yanga ikiwa bora msimu huu imefungwa na Simba ambayo haiku vizuri sana.

Geof Lea amesema hayo kufuatia Yanga kufungwa bao 2-0 na watani zao Simba katika Dimba la Mkapa juzi Jumapili Aprili 16, 2023.

“Ni kweli timu bora imefungwa na timu ya hamasa. Inafahamika kwamba Yanga ndiyo timu bora hapa nchini kwa sasa, kwanza ni mabingwa watetezi na wanaongoza Ligi. Kufungwa jana hakuzuii mapambano yao ya kusaka ubingwa mwaka huu.

“Kule Uingereza, Liverpool iliifunga Manchester United bao 7-0, lakini Liverpool ipo nyuma kwenye msimamo wa EPL ikilinganishwa na Man United. Ubora wakati mwingine unaweza ni wa jumla (general) au kutokana na siku husika ya mchezo.

“Ukiangalia mwenendo wa mchezo, umiliki wa Yanga ulikuja kipindi cha pili baada ya Simba kuwa wameshawaadhibu Yanga na hawana cha kupoteza kwa dakika zile lakini yanga hawaku-control mchezo wala kutengeneza nafasi.

“Kitu cha kwanza kwenye mchezo ni kufunga wala sio kumiliki, takwimu hizo zipo tu lakini kikubwa ni matokeo na kuondoka na alama tatu muhimu,” amesema Geof Lea.

SOMA NA HII  MSUVA AVUNJA UKIMYA DILI LAKE LA KUTUA YANGA...ADAI NI NYUMBANI...AFICHUA SIMBA WALIVYOMFUATA MARA TANO...