KISA KUNYUKWA NA SIMBA...MUSONDA ASHINDWA KUAMKA...AMEFUNGUKA HAYA
Habari za michezo

KISA KUNYUKWA NA SIMBA…MUSONDA ASHINDWA KUAMKA…AMEFUNGUKA HAYA

Marce Ben Komba April 18, 2023 3:17 pm

Mshambuliaji wa Yanga SC, Kennedy Musonda amewaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo kutokana na kipigo cha bao 2-0 kutoka kwa watani zao wa Jadi, Simba Sc uliopigwa juzi Aprili 16, 2023 katik dimba la Mkapa.

Musonda ambaye ni raia wa Zambia amewashukuru pia mashabiki wa klabu hiyo kwa kuendelea kuwasapoti huku akiahidi kuwa watarejea kwa nguvu na ari zaidi ili kutimiza malengo waliojiwekea katika msimu huu.

“Habari za asubuhi Wananchi, asanteni kwa sapoti yenu ya jana. (juzi), tumewaangusha na inauma sana, imekuwa ngumu kuamka leo baada ya kupoteza dabi yangu ya kwanza lakini tunawahitaji mashabiki zetu sasa kuliko hapo awali.

“Tumejifunza kutokana na makosa yetu na tutarudi tukiwa na nguvu na njaa zaidi ya mafanikio,” amesema Musonda.

KIBU DENIS AVUNJA REKODI HII YA KICHUYA…KATIKA MECHI YA SIMBA NA YANGA BAADA YA KUMALIZANA NA YANGA…SIMBA WAIGEUKIA WYDAD CA KWA HASIRA KALI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply