Habari za michezo
BAADA YA KUMALIZANA NA YANGA…SIMBA WAIGEUKIA WYDAD CA KWA HASIRA KALI
Marce Ben Komba
April 18, 2023
3:30 pm
Wekundu wa Mismbazi Simba SC, wamerejea kambini leo saa tatu asubuhi kuanza kambi kwa ajili ya kuwawinda Wydad Casablanca kutoka nchini Morocco.
Simba walipewa mapumziko ya siku moja mara baada ya kutoka kwenye mechi ya dabi dhidi ya Yanga SC na kuibuka na ushindi wa 2-0.
Akizungumza na wanahabari leo Apili 18, 2023, Afisa Habari wa Simba, Ahmed Ally alisema, nyota wote wanaingia kambini leo kwa ajili ya kuwawinda Wydad mchezo wa Klabu Bingwa hatua ya Robo Fainali ikiwa ni mechi ya kwanza itakayopigwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar majira ya saa 10:00 jioni.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.