Home Habari za michezo NABI AGEUKA MBOGO…AWARUKIA MAYELE NA MUSONDA…ISHU NZIMA HII HAPA

NABI AGEUKA MBOGO…AWARUKIA MAYELE NA MUSONDA…ISHU NZIMA HII HAPA

Tetesi za Usajili Yanga

Kocha Mkuu wa Young Africans Nasreddine Nabi amewataka Washambuliaji wake Fiston Mayele na Kennedy Musonda kuongeza umakini kwenye kutumia nafasi wanazopata ili kufunga mabao mengi katika michezo inayowakabili.

Young Africans bado inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 68 baada ya kucheza michezo 26, tofauti ya alama tano dhidi ya Simba SC inayoshika nafai ya pili kwa kuwa na alama 63.

Akizungumza kabla ya kuondoka jijini Dar es salaam mapema leo Alhamisi (Aprili 20) kuelekea nchini Nigeria, Nabi alisema kuna umuhimu kwa safu ya ushambuliaji kuongeza umakini na kutumia nafasi wanazopata kwenye kila mchezo.

“Unaona tumetoka kupoteza dhidi ya Simba SC, haina maana kwamba tulizidiwa sana, hapana, ilikuwa ni kushindwa kutumia nafasi ambazo tulipata hasa kipindi cha pili.”

“Kipindi cha kwanza ukweli tulivurugwa hasa kwa kufungwa bao la mapema ambalo lilitokana na kona, kuna kazi ya kufanya kwenye mechi zijazo hasa kuhakikisha nafasi ambazo tunapata kwa washambuliaji wetu wanafunga,” alisema Nabi.

Kwenye mchezo uliopita Aprili 16, mwaka huu dhidi ya Simba SC, Nabi alianza na washambuliaji wawili, Mayele na Musonda ambao majaribio yao yote yaligotea kwenye mikono ya kipa chaguo la tatu wa Simba, Ally Salim, mchezo ukaisha kwa Young Africans mabao 2-0.

Young Africans Jumapili (Aprili 23) itarejea katika Dimba la Ugenini nchini Nigeria kucheza mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Rivers United.

Timu hizo zitacheza mchezo wa Mkondo wa Pili April 30, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, na mshindi wa jumla atakayecheza Nusu Fainali atajulikana.

SOMA NA HII  BAADA YA KISINDA KURUHUSIWA ....MAMBO YABADILIKA YANGA...NABI AIBUKA NA MSIMAMO HUU ...