Simba SC vs Wydad
Habari za michezo

FT:- SIMBA 1-0 WYDAD….BALEKE AZIDI KUSHANGAZA SOKA LA TZ…WAARABU WAFURA KWA HASIRA…

admin April 22, 2023 6:10 pm

WAWAKILISHI Pekee Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati katika hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika Simba SC wameng’ara nyumbani baada ya kuichapa bao 1-0 Wydad Casablanca Athletic mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Shujaa wa Simba SC ni Mshambuliaji hatari katika Michuano hiyo Jean Baleke alifunga dakika ya 30 na bao hilo liliwapeleka wenyeji Mapumziko wakiwa wanaongoza.

Kwa ushindi huo Simba SC wataenda nchini Morocco katika marudiano wakiwa na bao moja hivyo kwenda kutafuta bao jingine au sare ili waweze kutinga hatua ya Nusu Fainali Aprili 29 watarudiana tena.

Wawakilishi katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika timu ya Yanga SC watashuka dimbani kesho kucheza na Rivers United nchini Nigeria

IFANYE EID YAKO KUWA TAMU KWA KUSHIKILIA ODDS ZENYE UJAZO KUTOKA MERIDIANBET… A-Z JINSI SIMBA SC WALIVYOIBAMBA WYDAD KWA MKAPA….ISHU NZIMA ILIANZAI HAPA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply