Home Habari za michezo HII HAPA IMEVUJA…KOCHA SIMBA ATAJA JINA LA WINGA HUYU…KUSAJILIWA MAPEMA TU

HII HAPA IMEVUJA…KOCHA SIMBA ATAJA JINA LA WINGA HUYU…KUSAJILIWA MAPEMA TU

Habari za Simba SC

JINA la kwanza lililopendekezwa na kocha wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ kusajiliwa pindi tu dirisha litakapofunguliwa ni winga wao wa zamani Hassan Dilunga ambaye ameshaanza kula matunda ya timu hiyo.

Mwaka mzima Dilunga alikuwa nje baada ya kuumia mazoezini, sasa ni miezi kadhaa imepita mchezaji huyo anafanya mazoezi na timu hiyo, jambo lililomshawishi kocha kukubali kiwango chake.

Mmoja wa kiongozi wa timu hiyo ambaye hakutaka jina lake liweke wazi (SOKA LA BONGO  tunalo), alisema ‘Robertinho‘ amewaambia viongozi kwamba ukianza usajili waanze na Dilunga anaona anamfaa kwenye kikosi chake.

“Kwenye mazoezi Dilunga anaonyesha kiwango cha juu, kinachomfanya kocha aamini ni kati ya wazawa ambao wanaweza wakawa msaada mkubwa ndani ya kikosi chake msimu ujao.

“Dilunga aliumia akiwa na Simba, ndio maana alipewa nafasi ya kufanya mazoezi na wenzake, pamoja na hilo mchezaji mwenyewe hakujibweteka anapenda mazoezi na alionyesha ana kitu kikubwa kinachomfanya kocha apende kumuona kwenye kikosi chake na nafakiri ameshawaambia uongozi kuwa anamhitaji kwa ajili ya msimu ujao, kama watawezana basi ataonekana kwenye jezi ya Simba.”

Kwenye nafasi ya Dilunga waliopo kwenye kiwango kwa sasa ndani ya Simba ni Clatous Chama na Saidi Ntibazonkiza ‘Saido‘, lakini ambao hawapati nafasi sana ni Pape Sakho anayepewa dakika chache, Peter Banda na Jimmyson Mwanuke ambao hawapati nafasi mara kwa mara.

Dilunga aliwahi kufanya makala na gazeti hilo na kusema kuwa anajitahidi kupambana kuonyesha kiwango chake, lakini hakimu wa mwisho kuamua kumrejesha kikosini ni kocha.

“Nashukuru nafanya nao mazoezi, binafsi napambana kuhakikisha kocha anakielewa kiwango changu, mengine namuachia mwenyewe,”alisema.

Kwa upande Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Simba, Ahmed Ally alisema; “Dilunga ni mwanafamilia wetu hivyo ni kweli kuna vitu huwa tunafanya kwake kama pale inapopatikana posho naye anapata, ili kumsaidia kwenye mambo yake madogo madogo, hata alikokuwa anafanya mazoezi ya kujiweka fiti tulikuwa tunamlipia.

“Kuhusu mapendekezo ya kocha kutaka kumsajili, kwangu halijafika ingawa Dilunga alitakiwa ajiunge nasi wakati wa Kombe la Mapunduzi lakini alitueleza kuwa bado hajawa fiti, ndiyo maana sasa hivi yupo na tumeliachia benchi la ufundi ndiyo wataamua pamoja na yeye kama ataona yupo fiti pale ambapo benchi litaona anafaa kumpa mkataba.”

SOMA NA HII  TAIFA STARS TAYARI KUIVAA ETHIOPIA