MSHAMBULIAJI HUYU WA BONGO...APEWA SHAVU UBELGIJI...KUKIPIGA NA SAMATTA
Ligi Kuu

MSHAMBULIAJI BONGO…APEWA SHAVU UBELGIJI…KUKIPIGA NA SAMATTA

Marce Ben Komba April 26, 2023 3:50 pm

Imeelezwa kuwa mshambuliaji wa Kagera Sugar, Anuary Jabir ‘Falcao’ ameongezewa muda zaidi wa majaribio kwenye klabu ya KAA Gent inayoshiriki Ligi Kuu Ubelgiji.

Awali mshambuliaji huyo aliyetua Ubelgiji tangu Aprili 04, mwaka huu alipewa programu ya majaribio na timu hiyo kwa majuma mawili lakini sasa ameongezewa muda kwa ajili ya kuangaliwa zaidi.

Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa maendeleo ya Falcao ni mazuri na kuna programu mpya amepewa ambayo ataifanya kwa siku chache ingawa hakueleza ni kwa kipindi cha muda gani.

“Anwar ameongezewa muda kule Ubelgiji, ni kweli majuma mawili yamekwisha lakini kuna programu nyingine ambayo wao wenyewe wametaka aifanye kwa muda kabla ya kumaliza rasmi majaribio yake.”

“Kwa kifupi anaendelea kufanya vizuri na sisi tumekuwa
tukimwombea aendelee kufanya hivyo na tunaamini programu aliyopewa sasa ndiyo itakuwa programu yake ya mwisho ambayo itafanyika kwa siku chache tu,” amesema Maxime.

Endapo Falcao atafaulu majaribio yake hayo atakuwa mchezaji wa nne Mtanzania kukipiga Ubelgiji baada ya nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta na Kelvin John wanaokipiga KRC Genk na Novatus Dismas wa Zulte Waregem.

TANZIA:KOCHA APATA AJALI YA GARI…AFARIKI DUNIA…KUZIKWA LEO HATIMAYE SIMBA…YAPATA MRITHI HUYU WA TSHABALALA…ATOBOA SIRI NZITO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply