Habari za michezo
TANZIA:KOCHA APATA AJALI YA GARI…AFARIKI DUNIA…KUZIKWA LEO
Marce Ben Komba
April 26, 2023
3:36 pm
Mwili wa Francis John, aliyekuwa kocha wa mwanariadha, Alphonce Simbu, utazikwa leo Aprili 26 nyumbani kwake jijini Arusha.
Francis alifariki jioni ya Jumamosi iliyopita kwa ajali ya gari. Simbu ameiambia SOKA LA BONGO kuwa maziko ya kocha huyo yatafanyika kwenye eneo la nyumba yake huko Arusha, mchana huu.
Hadi mauti inamkuta, Francis alikuwa kocha binafsi wa mwanariadha huyo ambaye pia ni mshindi wa medali ya shaba ya Jumuiya ya Madola.
Mbali na ukocha, Francis amewahi kuwa mwenyekiti wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT).
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.