Home Habari za michezo ALLY SALIM AWEKA REKODI HII MPYA KWA SIMBA SC…SI MANULA WALA KAKOLANYA...

ALLY SALIM AWEKA REKODI HII MPYA KWA SIMBA SC…SI MANULA WALA KAKOLANYA WANGEWEZA…

Habari za Simba SC

Malinda Lango chaguo la Tatu Simba SC Ally Salim ameweka Rekodi ndani ya kikosi cha klabu hiyo baada ya kufanikiwa kucheza dabi yake ya kwanza akionyesha kiwango cha juu katika kuzuia mashambulizi ya Washambuliaji wa Yanga wakiongozwa na Fiston Kalala Mayele.

Salim ambaye aliwashtua wengi baada ya kuonekana katika kikois cha kwanza cha Simba SC kilichoikabili Yanga juzi Jumapili (April 16) Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, akichukuwa nafasi ya Aishi Manula na Beno Kakolanya.

Kipa huyo licha ya huo kuwa ndiyo mchezo wake wa kwanza wa dabi lakini alionyesha kiwango cha juu katika kulizuia lango lisiweze kufungwa na washambuliaji wa Yanga na aliweza kumaliza mchezo huo bila ya kuruhusu bao.

Huo ni mchezo wa pili kwa Salim kucheza kwa msimu huu akiwa na Simba SC baada ya awali kucheza dhidi ya Ihefu SC jijini Mbeya na kufanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 huku akimaliza mchezo huo bila ya kuruhusu bao β€˜clean sheet’.

SOMA NA HII  KISA YANGA KUTINGA FAINAL CAF....WACHINA BONGO WATOA TAMKO LAO...