Home Habari za michezo FT: RIVER UTD 0-2 YANGA SC…..MWAMNYETO AANZA KUVAA VIATU VYA FEI TOTO….’WANIGERIA...

FT: RIVER UTD 0-2 YANGA SC…..MWAMNYETO AANZA KUVAA VIATU VYA FEI TOTO….’WANIGERIA WAFURA’…

River vs Yanga SC

WAWAKILISHI Pekee ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Timu ya Yanga SC wamelipa kisasi baada ya kuwachapa mabao 2-0 wenyeji Rivers United mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika hatua Robo ya Fainali mchezo huo umepigwa katika uwanja wa Godswill Akpabio nchini Nigeria.

Kipindi cha kwanza timu zote zilienda mapumziko zikiwa hazijafungana huku wenyeji wakimiliki mpira kutokana na Yanga SC kuanza na viungo wengi na mabeki.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko yaliyoweza kuipa Yanga ushindi huo mnamo dakika ya 74 Mshambuliaji hatari kwa sasa ndani na nje ya nchi Fiston Mayele alifunga bao la kwanza akimalizia pasi ya Nahodha wake Bakar Mwamnyeto.

Rivers wakiwa wanawaza kusawazisha bao Yanga SC walipiga counter yule yule mtoa pasi Bakar Mwamnyeto alimpa tena Fiston Mayele dakika ya 81 na kufunga bao la pili likiwa bao lake la tano na kuwa kinara katika kufumania nyavu katika Michuano hiyo

Kwa matokeo hayo Yanga SC imejiweka katika mazingira mazuri ya kutinga Nusu Fainali kwani inahitaji kulinda tu ushindi wake hata wakifungwa bao moja watafuzu hatua hiyo timu hizo zinatarajia kurudiana kati ya Aprili 29 au 30,mwaka huu.

SOMA NA HII  FEI TOTO APEWA NAMBA NDANI YA KIKOSI CHA SIMBA