Home Habari za michezo KUHUSU ONYANGO KUCHEZA MECHI NA YANGA KESHO KUTWA…EDO KUMWEMBE AIBUKA NA HILI...

KUHUSU ONYANGO KUCHEZA MECHI NA YANGA KESHO KUTWA…EDO KUMWEMBE AIBUKA NA HILI JIPYA…

Habari za Simba

Wakati wengi wakionekana kuwa na mashaka na kiwango cha Beki Mkenya Joash Onyango kuelekea mchezo wa Dabi ya Kariakoo Aprili 16.

Mchambuzi kutoka Wasafi Fm Edo Kumwembe amesema makosa aliyoyafanya Onyango kwenye mechi za kimataifa hayawezi kumfanya akose nafasi kwenye mechi ya Kariakoo Derby kwa sababu makosa hayo aliyafanya wakati akiwa kwenye Timu zenye kiwango kikubwa.

“Onyango tumuache kwenye hayo makosa kwa sababu yalikuwa ni kwenye Top Level ni Against Raja mjue, Raja sio Yanga asikudanyanye mtu, wanaweza kuwa wazuri lakini Raja sio yanga.

“Kwani Onyango si anacheza kila siku hayo makosa kafanya? Onyango kamdhibiti Mayele mara ngapi ?, si tulikuwa tunamsifu hapa kwa kumdhibiti Mayele,”

Simba wataikaribisha Yanga katika Uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumapili mchezo wa mzunguko wa pili Ligi Kuu ya NBC.

SOMA NA HII  MABILIONI YA CAF 'YAPIGWA PANGA' SIMBA, YANGA....MASTAA KUAMBULIA MGAO HUU....ISHU HII HAPA...