Home Habari za michezo MAYELE “NILIKUWA NAWATAMANI SANA RIVERS…WALITUTOA MAPEMA WAKAONGEA SANA

MAYELE “NILIKUWA NAWATAMANI SANA RIVERS…WALITUTOA MAPEMA WAKAONGEA SANA

Habari za Yanga SC

Mshambuliaji kinara wa Yanga, Fiston Kalala Mayele amesema kuwa alikuwa akitamani kukutana na timu ya Rivers United ya Nigeria katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, jambo ambalo limetimia.

Mayele ametoa kauli hiyo mara baada ya yanga kupangwa kukutana na Rivers katika hatua hiyo huku Wananchi wakiwa na kumbukumbu ya kuondolewa na Rivers katika hatua ya awali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika msimu uliopita (2021/22) baada ya kufungwa bao 1-0 nyumbani kisha wakaenda kufungwa bao 1-0 ugenini.

“Mimi binafsi nilikuwa namtaka (Rivers United) kwa sababu mwaka jana sikupata nafasi ya kucheza naye, tulitolewa mapema watu wakaongea sana kwa hiyo tumempata Sehemu nzuri na wakati sahihi,” amesema Mayele.

Itakumbuiwa kuwa, wachezaji wa Yanga, Fiston Mayele, Khalid Aucho na Djuma Shabani, hawakucheza dhidi ya klabu ya Rivers Utd msimu uliopita katika raundi ya kwanza ya CAF Champions League kwa sababu walichelewa kupata (ITC) zao baada ya kusajiliwa na klabu hiyo.

SOMA NA HII  MAXI NZENGELI ATAMBA NA REKODI YA MAYELE