Home Habari za michezo PITSO MOSIMANE AKARIBIA LIGI KUU….ISHU NZIMA IKO NAMNA HII….

PITSO MOSIMANE AKARIBIA LIGI KUU….ISHU NZIMA IKO NAMNA HII….

Pitso Mosimane

Kocha Pitso Mosimane anaendelea kuweka heshima huko Saudi Arabia katika Ligi Daraja la kwanza baada ya kukaribia kuirejesha Ligi Kuu Klabu ya Al Ahli Saudi Football Club.

Hapo jana wameichapa Al Ain bao Kwa Nunge na kukaa kileleni mwa msimamo wa Saudi Division 1 wakifikisha alama 58 wakimwacha Al Akhdoud nafasi ya pili akiwa na alama 56 huku nafasi Al Hazem akiwa nafasi ya tatu akiwa na pointi 55 huku nafasi ya Nne ikienda Kwa Al Riyadh’s aliyekusanya alama 53 Kibindoni.

Hadi sasa timu zote zimeshashuka Dimbani mara 27 ila Kuna mchuano mkali Kwa timu zilizopo top 4 yoyote ana nafasi ya kumaliza kinara wa Division 1 licha ya kuwa Al Ahli SC ni vinara ikiwa imesalia michezo Saba.

Mosimane aliikuta timu hii ikiwa katika nyakati ngumu sana ila Kwa sasa Kila kitu imebaki story bao la Jana limefungwa na nyota wao Amaral dakika ya tisini.

Mchezo huu zilitoka kadi nyekundu tatu Moja ikienda Kwa Al Ahli SC huku Al Ain wakisepa nazo mbili ndani ya Dakika tisini.

Al Ahli 1️⃣-0️⃣ Al Ain.

SOMA NA HII  ALIYETUPIA 'HAT TRICK' ATUMA SALAMU YANGA...ATOA ONYO KUHUSU MTEREMKO....