Home Habari za michezo WAMEKWISHAA…..NABI ATUA BONGO NA ‘FAILI’ LA MASTAA 6 HATARI WA RIVER UTD….KAZI...

WAMEKWISHAA…..NABI ATUA BONGO NA ‘FAILI’ LA MASTAA 6 HATARI WA RIVER UTD….KAZI KUIANZA NA SIMBA…

Habari za Yanga SC

WAUMINI wa madhehebu ya Kikristo wakisheherekea sikukuu ya Pasaka leo, Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi atakuwa kwenye ardhi ya Dar es Salaam akiwa na faili lenye siri za mastaa sita wa River United mkononi. Ameliambia Mwanaspoti kwamba ana dondoo za kutosha mkononi.

Yanga imepangwa kukiwasha na timu hiyo ya Nigeria kwenye mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika Aprili 23 ugenini kabla ya kurejeana Dar es Salaam. Nabi alikuwa kwao Ubelgiji kufuatilia hati mpya ya kusafiria.

Nabi amesema kuwa ameanza kazi ya kuicheza mechi hiyo na amegundua msimu huu Wanigeria hao nusu ya wachezaji ni wapya tofauti na ile aliyokutana nao mara ya mwisho Septemba 19, 2021. Yanga ilipasuka nje ndani kwa bao 1-0.

Nabi ametamka kwamba hata kama wanataka kulipa kisasi, lakini hautakuwa mchezo rahisi kwa vile Rivers itakuwa timu mpya ambayo ni lazima wajipange kiakili kuivamia.

Nabi alisema tayari benchi la ufundi limeshaanza hesabu za kuifuatilia Rivers na faili nzima la timu hiyo limekabidhiwa kwa mtaalam wa kuchambua mikanda ya wapinzani, Khalil Ben Youssef.

Katika kikosi cha mwisho ambacho Rivers ilikutana na Nabi anasema kina wachezaji 6 tu waliocheza mchezo huo wa 2021-2022 na watano wanaanza kikosi cha kwanza cha sasa.

Kwa msimu huu kikosi kilichocheza hatua ya makundi na kumaliza nafasi ya pili katika Kundi B Vipers inawatumia kipa Victor Sochima, beki wa kulia Kazie Godswill, beki wa kushoto Eduba Dum, mshambuliaji Malachi Ohawume, kiungo mshambuliaji na kinara wa ufungaji Paul Acquah na kiungo mkabaji Morice Chukwu aliyeingia kikosi cha kwanza msimu huu, huku benchi ikiwa na kipa Darlington Ovunda.

Mastaa wapya watano ambao wamo katika kikosi hicho sasa ni pamoja na mabeki wao wa kati wawili Ngwen Ndasi, Lawrence Edward, viungo wa kati Joseph Onoja, Ukeme Williams na mshambulaiji Nyima Nwagua huku kocha wao akibaki kuwa yule yule Stanley Eguma.

“Ni timu inayotakiwa kuipa heshima kwa kuhakikisha tunajipanga vizuri kabla ya kukutana nao, nimeangalia naona ni timu mpya kabisa kama ilivyo sisi , kila timu iliyofika hatua hii inatakiwa kupewa heshima nadhani tutajipanga vizuri tayari kwa mchezo huu,”alisema Nabi ambaye amekuwa akihusishwa na kujiunga na TP Mazembe ambayo imepoteza uelekeo.

Wakati Nabi akiyasema hayo kikosi chake kilichocheza mchezo huo wa mwisho na Rivers United kimebakiza wachezaji watano pekee waliopo kikosi cha kwanza cha sasa, huku wanne wengine wakiwa wanatokea benchi wakati mmoja akiwa nje ya kikosi hicho.

Wanaoanza sasa ni kipa namba moja Djigui Diarra, kiungo kiraka Yannick Bangala, mabeki Dickson Job na Bakari Mwamnyeto na winga Jesus Moloko.

Wengine waliokuwepo katika mchezo huo wa mwisho ambao sasa wamepoteza nafasi ni beki Kibwana Shomari, kiungo Feisal Salum ambaye yuko nje ya kikosi hicho, huku beki Abdallah Shaibu, kiungo Zawadi Mauya, mawinga Dickson Ambundo na Farid Mussa waklianzia benchi kila mara.

Yanga itaringia pia mastaa wapya sita ambao hawakucheza mechi ya mwisho ya Rivers akiwemo beki wa kulia Djuma Shaban, beki wa kushoto Joyce Lomalisa, beki wa kati Ibrahim Abdullah ‘Bacca’ kiungo mkabaji Khalid Aucho, na washambuliaji Fiston Mayele na Kennedy Musonda.

SOMA NA HII  KUMBE!METACHA ANAWADAI YANGA,NYOTA MNIGERIA AKUBALI KUTUA SIMBA, CHAMPIONI JUMAMOSI