Home Habari za michezo WYDAD – TULIKUWA TUNAWATAKA SANA SIMBA…TUNAKUJA TZ KUMALIZA MCHEZO MAPEMA TU…

WYDAD – TULIKUWA TUNAWATAKA SANA SIMBA…TUNAKUJA TZ KUMALIZA MCHEZO MAPEMA TU…

Habari za Simba SC

Msemaji wa Mabingwa wa Soka Barani Afrika Wydad athletic Club Mahmoud sheriff ameitumia salamu Simba SC baada ya kupangwa kwa Droo ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Shirikisho la Soka Afrika ‘CAF’ Jumatano (April 05) lilipanga Droo ya Robo Fainali ya Ligi Ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Barani humo, huku Simba SC ikiangukia mbele ya Mabingwa Wydad AC na Young Africans ikipelekwa Nigeria kupapatuana na Rivers United.

Sherrif amesema: “Sisi kama Wyadad Athletic Club malengo yetu nikutetea taji letu hili kuhakikisha kwamba tunalibakisha Nchini hapa (Morocco), nipende kukutoa hofu tu kwamba hatuiogipi Simba SC hata kidogo bali tunaiheshimu kama timu kubwa Afrika.

“Tunawajua vyema Simba SC ni timu nzuri hasa linapokuja suala la kutumia vyema uwanja wao wa nyumbani, hakika nikiri tu wapo vizuri kwenye dimba lao la nyumbani.”

“Licha ya hayo lakini niwakumbushe tu kuwa sisi ndo watawala wa Soka la Afrika kwa sasa, Simba SC uwezo wa kumpiga nje ndani tunao, uwezo wa kumaliza game wakiwa kwao tunao, hivyo niwatoe hofu tu mashabiki wa Waydad Nusu Final ni swala la muda tu kwetu”

“Baada ya kuona tumepangwa na Simba SC kwenye Droo ile wachezaji wetu wote nimeona wakifurahi kwa tabasamu na bashasha liliwajaa kwenye nyuso zao hii unafikiri ni kwasababu yanini? hii nikwasababu kwamba tulikua tunamtaka sana Simba SC na malengo yetu yametimia”

“Mpaka sasa tunawafuatilia kwa ukaribu sana Simba SC tupo nyuma yao kwa kila hatua wafanyayo, game yao ya Ijumaa tumeoiona, ni timu nzuri na soka safi wanalionyesha ila tu niseme watatusamehe tukiwa na jambo letu”

“Nimepata wasaa wa kuongea na Akroum binzou (Mshambuliaji hatari wa Wydad) yeye alichonijibu ni kwamba hakika Wydad inaenda kuumaliza mchezo Tanzania kabla ya kurudi Morocco.”

“We are wydad Athletic club we are coming Tanzania soon”

Mchezo wa Robo Fainali Mkondo wa kwanza umepangwa kupigwa jijini Dar es salaam katika Uwanja wa Mkapa April 21-22, huku mchezo wa Mkondo wapili ukipangwa kuunguruma mjini Casablanca-Morocco kwenye Dimba la Mohammed V April 28-29.

SOMA NA HII  WAKATI SAKHO AKIFANYA MAAJABU HUKO...MUGALU AMTAZAMA WEE..KISHA ASEMA YEYE NI MAYELE TU...