Home Azam FC KUELEKEA MECHI YA SIMBA vs AZAM KESHO….JE YA MIQUISSONE KUJIRUDIA TENA..?

KUELEKEA MECHI YA SIMBA vs AZAM KESHO….JE YA MIQUISSONE KUJIRUDIA TENA..?

Simba vs Azam

Mwishoni mwa wiki hii Simba na Azam zinakutana kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara ikiwa ni mchezo wa nusu fainali Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ambapo Yanga ndio bingwa mtetezi.

Timu hizo zinakwenda kukutana zikiwa na kumbukumbu ya mchezo wa nusu fainali iliyopita ambayo ilichezwa Uwanja wa Majimaji Julai 26, 2021 na Simba kushinda bao 1-0 lililofungwa na Luis Miquissone.

Baada ya hapo, Simba na Azam zimekuwa zikikutana kwenye Ligi Kuu pekee ambapo tangu Julai 26, 2021 zimekutana mara nne, Simba ikishinda michezo mitatu na Azam ikishinda mchezo mmoja kwa bao 1-0 hiyo ilikuwa Oktoba 27, 2022.

Nje ya Ligi Kuu zimekutana mara moja kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi Januari 13, 2022 na dakika 90 kumalizika Simba ikishinda bao 1-0 lililofungwa na Meddie Kagere.

Hata hivyo, historia ya timu hizo tangu mwaka 2015 Azam ikishiriki Ligi Kuu kwa mara ya kwanza zimekutana mara tatu ndani ya Mei na mara zote hakuna mbabe. Mara ya kwanza zilikutana Mei 1, 2016 kwenye mchezo wa Ligi

Kuu na timu hizo kutoka suluhu, mara ya pili zilikutana Mei 13, 2019 mchezo wa Kombe la Mapinduzi na kutoka suluhu, kisha zikakutana Mei 18,2022 na kutoka sare ya bao 1-1 ukiwa mchezo wa Ligi Kuu.

Rekodi zinaonyesha nje ya Ligi Kuu timu hizo zimekutana mara nne, huku rekodi zinaibabe zaidi Simba kwani kwenye Ligi Kuu katika michezo 16 imeshinda michezo sita, sare nane na ikipoteza michezo miwili.

Mapinduzi Cup zimekutana mara tatu, Simba ikishinda mara mbili na sare moja wakati Kombe la Kagame zikikutana mara moja na Azam ikishinda mabao 2-1 huku ASFC zikikutana mara moja na Simba kushinda bao 1-0.

Msimu huu Simba imepoteza mchezo mmoja pekee ilipopoteza bao 1-0 dhidi ya Azam Oktoba 27, 2022 bao lililofungwa na Prince Dube baada ya hapo Simba imedondosha alama kwa kupata sare.

Beki wa zamani wa Simba, Azizi Nyoni alisema mwendelezo mzuri wa matokeo ya Simba inawapa nafasi kubwa kupata ushindi kwenye mchezo huo.

“Simba imekuwa na matokeo mazuri kwenye michezo yake hivi karibuni lakini hili ndio kombe naweza kusema ambalo Simba inalitolea macho kwa sasa maana lile la ligi bado kuna mlima mkubwa.

“Hata hivyo Azam na Simba zinapokutana unakuwa mchezo mgumu kutokana na aina ya wachezaji ambao wanao hivyo atakayekuwa na siku nzuri ndio atapata matokeo mazuri siku hiyo,” alisema Nyoni.

Tangu ASFC iliporejeshwa mwaka 2015, Simba imebeba ubingwa mara tatu, 2016/17, 2019/20 na msimu wa mwaka 2020/21 wakati Yanga ikibeba mara mbili 2015/16, na 2021/22, Mtibwa 2017/18 na Azam msimu wa mwaka 2018/19.

Naye kocha wa Azam Kally Ongala alisema; “Michezo ya mtoano huwa siku zote ni migumu kwa sababu ni mechi moja tu, tunatambua ubora wao lakini sisi malengo yetu kama timu na klabu ni kuhakikisha msimu huu tunamaliza na taji moja, “Tuna kumbukumbu ya mechi ya mwisho ya hatua kama hii wakati tunakutana na Simba hivyo ni wakati kwetu wa kulipa kisasi.”

SOMA NA HII  RIPOTI KUTOKA CAF KUHUSU BIASHARA UNITED IKO HIVI...