Maruno Gallants
Habari za michezo

WASAUZI WAIFANYIA YANGA UMAFIA….WATUMA MASHUSHU 7 KUJA KUMALIZA KILA KITU MAPEMA…

admin May 6, 2023 3:36 pm

Imeelezwa kuwa wapinzani wa Yanga SC katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika, Marumo Gallants, wametuma jeshi la watu saba kusoma mazingira ya jiji la Dar es salaam, Tanzania.

Yanga SC itakuwa mwenyeji wa mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika Mei 10 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, kabla ya mchezo wa Mkondo wa Pili utakaopigwa Afrika Kusini Mei 17, kwenye Uwanja wa Dobsonville jijini Johannesburg.

Taarifa kutoka Afrika Kusini zinaeleza: “Mafanikio ya Marumo kwenye mechi zote za ugenini yalitokana na ujanja wao wa kupenyeza watu kwa kuhakikisha wanatuma timu kubwa mapema ili iweze kusoma mazingira yote ya wapinzani wao kabla ya timu kuwasili.

“Walifanya hivyo tangu mwanzo na hiyo imekuwa ni silaha yao kubwa, ambapo ile timu imekuwa na kawaida ya kijipenyeza maeneo yote ya wapinzani wao, kisha wanatuma ripoti ikiwa sambamba na kuona viwanja vya mazoezi na ule wa mchezo.”

Marumo Gallants ilitinga Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa kuifunga Pyramid ya Misri kwa ushindi wa jumla wa 2-1, huku Young Africans ikiitupa nje Rivers United ya Nigeria kwa ushindi wa jumla wa 2-0.

KUELEKEA MECHI NA SIMBA KESHO….MABOSI AZAM FC WAAMUA KUFANYA UAMUZI HUU MGUMU…. KUELEKEA MECHI YA SIMBA vs AZAM KESHO….JE YA MIQUISSONE KUJIRUDIA TENA..?

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply