Habari za Simba leo
Habari za michezo

KUHUSU ISHU YA MANULA KUWA NNJE MSIMU MZIMA…UKWELI HALISI NI HUU HAPA…

admin May 6, 2023 11:39 am

Kipa namba moja wa Simba SC, Aishi Salum Manura atakosekana kwenye michezo iliyosalia katika mashindano yote mpaka mwisho wa msimu huu.

Hayo yameelezwa na Meneja wa Habari na mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally wakati akizungumza na wanahabari mjini Mtwara ambako timu hiyo imeweka kambi kujiandaa na mechi ya nusu fainali ya Kombe la shirikisho dhidi ya Azam FC.

“Nyota wetu wote wapo vizuri na timamu ila mchezaji ambaye bado ni majeruhi ni Aishi Manula ambaye yeye kuna uwezekano mkubwa akakosekana hadi mwisho wa msimu, lakini vilevile Mohammed Ouattara naye bado anasumbuliwa na majeraha”

“Lakini nyota wengine wote simba tupo nao hapa rwangwa na wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu wa nusu fainali dhidi ya Azam FC,” amesema Ahemd Ally.

Simba sasa wamelazimika kuanza kumpa mazoezi kipa namba nne Ahmad Feruz ili kusaidiana na kipa namba tatu, Ally Salim baada ya Beno Kakolanya kuwa na changamoto ya kimkataba na klabu yake huku akihusishwa kusaini Singida Big Stars.

Manula anasumbuliwa na tatizo la nyonga mabapo mpaka sasa amekosa mechi sita mpaka sasa kutokana na tatizo hilo.

MBRAZILI SIMBA AANDAA PANGA ZITO…MASTAA HAWA KUPIGWA CHINI…NABI AKABIDHIWA BRUNO…. KUELEKEA MECHI NA SIMBA KESHO….MABOSI AZAM FC WAAMUA KUFANYA UAMUZI HUU MGUMU….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply