Habari za michezo
ILI KUEPUKANA NA ‘FIGISU FIGISU’ ZA YANGA….WASAUZI WAAMUA ‘KUUCHUNA’…’WASUSA’ KILA KITU BONGO…
admin
May 9, 2023
10:46 am
Klabu ya Marumo Gallants kutoka Afrika Kusini ambayo itachuana na Yanga kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza kombe la Shirikisho barani Afrika bado haijafanya mawasiliano na wenyeji wake, Klabu ya Yanga.
Kwa mujibu wa kanuni za CAF, Yanga ikiwa mwenyeji wa mchezo huo ina jukumu la kuwapokea wageni wao na kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu ikiwa ni pamoja na kuwapa usafiri kutoka uwanja wa Ndege mpaka hoteli watakayofikia
Afisa habari wa Yanga Ally Kamwe amesema klabu imefanya jitihada muhimu za kuwasiliana ma Marumo lakini hawajajibu wala kutoa taarifa juu ya ujio wao
Hata hivyo Kamwe amesema wanazo taarifa ambazo sio rasmi kuwa klabu hiyo huenda ikawasili nchini mapema Jumanne ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo dhidi ya Yanga
“Ni kweli hatuna taarifa za ujio wa Marumo Gallants. Tuliwaandikia barua kuuliza wanakuja lini Tanzania hili ni jambo la kikanuni kabisa lakini hawakujibu hivyo mpaka sasa hatujui wanakuja lini. Ila za ndani kabisa baada ya kufanya research yetu tumebaini watakuja kesho Asubuhi,” alisema Kamwe.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.