Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA MBEGU KUTUA SIMBA MSIMU UJAO….IHEFU WAIBUKA NA MSIMAMO HUU…

KUHUSU ISHU YA MBEGU KUTUA SIMBA MSIMU UJAO….IHEFU WAIBUKA NA MSIMAMO HUU…

Habari za Usajili Simba SC

Wakati beki wa kushoto wa Ihefu, Yahya Mbegu akitajwa kutua Simba msimu ujao, benchi la ufundi la timu hiyo limesema uamuzi wa kubaki kikosini au kutimka kwa staa huyo upo mikononi mwake kwani mpira ni maisha.

Mbegu aliyewahi kuzitumikia Mwadui, Polisi Tanzania na Geita Gold, kwa sasa anakiwasha Ihefu na amekuwa na kiwango bora hadi kuitwa timu ya Taifa ya vijana (U20).

Kwa sasa beki huyo anatajwa kumalizana na Simba ili kuongeza nguvu kwenye beki ya kushoto inayochezwa zaidi na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na mkataba wake na Ihefu unaisha mwishoni mwa msimu huu.

Akizungumza kocha msaidizi wa timu hiyo, Zuberi Katwila alisema bado nyota huyo wanamhitaji lakini kama atahitaji kuondoka kupata changamoto mpya hawawezi kumzuia.

Alisema kimsingi ni kujali mkataba wake na timu yake kwa sasa na kama ataamua kuongeza au kutoongeza uamuzi ni wake kwani soka la sasa ni maisha na nyota huyo uwezo anao uwanjani.

“Sisi tunamhitaji ndio maana tulimsajili, uwezo anao ila hatuwezi kumzuia kwa sababu soka ni maisha, akiamua kuongeza muda Ihefu sawa, asipoamua bado ni haki yake,” alisema Katwila.

Kocha huyo aliongeza, kwa sasa bado hawajaanza mipango yoyote ya usajili japokuwa wanajiandaa kuanza kushawishi mastaa wao wanaomaliza mikataba kubaki.

“Bado hatujaanza ishu za usajili tunaendelea na maandalizi ya mechi tatu zilizobaki kuhakikisha tunashinda na kubaki salama ligi kuu ila tutajitahidi kushawishi wanaomaliza kuongeza mikataba,” alisema kocha huyo.

SOMA NA HII  KUELEKEA KARIAKOO DABI....MANULA AIPASUA SIMBA...MABOSI WAHAHA KUFANYA JAMBO...