Msemaji wa Klabu ya Yanga ambaye amefungiwa kujihusisha na masuala ya Soka, Haji Manara ametoa ushauri kwa klabu yake kuelekea mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger.
Ameandika Haji Manara; Sehemu ya kwanza ya mawazo yangu kuelekea fainali ya YANGA vs USM ALGIERS.
Mwaka 1991 fainali ya Klabu Bingwa Afrika ilikuwa Sports Club Villa ya Uganda na Club Africain ya Tunisia, timu yenye Washabiki wengi zaidi nchini Tunisia ambayo ilitolewa na Yanga msimu huu.
Kabla ya mechi ya fainali hiyo kulikuwa na presha nchi nzima ya Uganda, Waganda walilitaka kombe, FA yao na Serikali nzima hadithi ilikuwa ni kombe la Ubingwa wa Afrika, Waliiamini Team yao iliyokuwa bora kweli kweli.
Majidu Musisi,Sule kato,William Nkemba,Sam Kabugo,Geofrey Higenyi ,Idi Batambuze na Captain wao Paul Hasule walikuwa Wachezaji mashuhuri na mahiri wa SC Villa na kila mmoja aliamini wanakwenda kushinda hyo mechi.
Mawaziri,Wabunge na hata Wafanyabiashara wakubwa walikuwa wanapishana kwenye Camp ya Villa kuwatia moyo Wachezaji na kutoa Ahadi za kila aina, ilikuwa ni presha tupu kwa Wachezaji, ni kama vurugu hivi ndani ya Camp yao, inatajwa hata muda wa mazoezi ukawa hautoshi kupisha ahadi na hotuba za kuwapa moyo.
Matokeo ya mwisho unayajua? Vila kwenda Tunis akafungwa 6-2 ,Kampala mechi ikaisha 1-1, hatimae Villa ya kina Musisi ikakosa fursa ya kuwa Club ya kwanza Afrika Mashariki kushinda Tittle ya Club Champions wa Afrika.
Even Makolo mwaka 1993 kwenye lile kombe la Abiola, sababu ya kufungwa katika fainali na Stella Abidjan ni Presha kubwa kambini toka Kwa kila Mtu maarufu, kambini hakukuwa na utulivu,hotuba zilikuwa nyingi kuliko Bungeni, Matajiri waliungana kuongeza ahadi, hata mazoezi yalifanyika kwa maelekezo ya FAT( TFF).
Sijui kama mnajua before the Kick off pale Uhuru Stadium ( Taifa zamani) ilitolewa hadi ratiba ya Kombe litapita barabara zipi? Zilianza Sherehe kabla ya mechi, Hadi kanga za ubingwa zilishatayarishwa, matokeo yake mechi imeisha Stella 2 Makolo 0, Makolo wakakosa Kombe mbele ya Rais Mwinyi.
Nisingetamani makosa hayo yajirudie,, tusitoe Presha Kwa team, tuwaache na maandalizi yao ya kawaida,Yes tunategemea support kubwa ya Wadau wakubwa wa football ,ila bila kubadili mwelekeo wetu ktk preparation za mechi.
Kwangu ni kuendelea kubaki Avic bila hotuba nyingi za kila mdau , kwangu fainali hii sio Do Or Die, kwangu mimi hatupaswi kubadili chochote.