Tetesi za Usajili
Habari za michezo

ILE ISHU YA SAOTHAMPTON YA UINGEREZA KUTAKA KUMSAJILI MTZ NOVATUS IKO HIVI….

admin May 29, 2023 2:22 am

Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Mail, Timu ya Southampton na Middlesbrough wameonesha nia ya kumsajili Novatus Dismas Miroshi kutoka klabu ya Zulte Waregem ya Ubelgiji.

Novatus mwenye umri wa miaka 20 alijiunga na Zulte msimu uliopita kutoka nchini Israeli, lakini ameendelea kuvutia kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi nyingi uwanjani.

Msimu huu Novatus amecheza kama kiungo, beki wa kushoto na wakati mwingine beki wa kati kwenye mfumo wa back three.

Licha ya timu yake kushuka daraja bado Miroshi ameendelea kuvivutia vilabu vikubwa.

Msimu huu Novatus amecheza michezo 36 akiwa na Zulte Waregem na kutoa pasi mbili za magoli huku akiichezea Taifa Stars na kufunga mabao mawili.

AUSSEMS ‘AMKUNA’ MTU HUKO…. BAADA YA KUCHAPWA JANA…INJINI HERSI ‘CHAP HARAKA’ AITA MKUTANO WA WANACHAMA YANGA…AJENDA HIZI HAPA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply