Home Habari za michezo FT: SIMBA 3-0 RUVU SHOOTING….CHAMA, SAKHO WAPELEKA KILIO KWA ‘WAJEDA’…

FT: SIMBA 3-0 RUVU SHOOTING….CHAMA, SAKHO WAPELEKA KILIO KWA ‘WAJEDA’…

Simba vs Ruvu Shooting

KICHAPO Cha mabao 3-0 ilichokipata Ruvu Shooting kutoka kwa Simba usiku wa leo kimeifanya timu hiyo kushuka daraja hadi Championship kimahesabu.

Katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Azam Complex, mabao ya Simba yamefungwa na Clatous Chama dakika ya 30 na Pape Sakho aliyefunga mawili dakika ya 72 na 90.

Kimahesabu Ruvu imeshuka daraja kwani imesalia mkiani na alama 20 huku ikiwa imebakiwa na mechi mbili mkononi ambazo hata ikishinda itafikisha alama 26 ambazo ni pungufu kwa Mbeya City iliyo nafasi ya 14 na alama 27 ikiwa imebakiza mechi tatu.

Kwa maana matokeo yeyote itakayoyapata Ruvu katika mechi mbili zilizosalia hayatsivusha katika nafasi mbili za mkiani kwa maanz ya 16 na 15 hivyo itashuka daraja moja kwa moja.

Ikumbukwe moja ya sheria za Ligi Kuu ni kushuka daraja moja kwa moja kwa timu mbili zitakazomaliza mkiani huku zile zitakazoishia nafasi za 13 na 14 kuamuliwa na mechi za mtoano ‘Play Off’.

Mechi mbili za mwisho za Ruvu itacheza na timu za kanda ya kati kwa maana ya Singida Big Stars iliyojihakikishia kumaliza katiks nafasi nne za juu kwenye msimano pamoja na Dodoma Jiji inayohaha kutocheza Play Off.

Pamoja na mabao ya Chama na Sakho mawili kuishusha daraja Ruvu, lakini pia yamewaongezea namba ambapo kwa Chama limekuws bao lake la nne msimu huu huku Sakho akifikisha tisa.

Pia pasi ya mwisho aliyoitoa Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ ikizaa bao la kwanza lilowekwa nyavuni na Chama ni ya sita kwake msimu huu akimfikia beki mwenzake wa Simba Shomari Kapombe na kuwafanya kuwa mabeki wenye asisti nyingi (6), hadi sasa kwenye ligi.

Pia pasi mbili za mwisho za Saidi Ntibanzokiza ziilizozaa bao la pili na la tatu kwa Simba yakifungwa na Sakho, zimemfanya kufikisha asisti 12 na kuwa mchezaji aliyehusika kwenye mabao mengi zaidi (22) katika ligi kwani ameasisti mara 12 na kufunga mabao 10.

Wakati leo Ruvu ikishuka daraja, kesho Yanga inaweza kutangazwa kuwa bingwa wa msimu huu kama itashinda mechi yake dhidi ya Dodoma Jiji kwani itafikisha alama 74, ambazo hakuna timu ya ligi kuu msimu huu inaweza kuzifikia.

Licha ya kishinda lakini Simba imesalia katika nafasi ya pili na alama 67 ikiwa imebakisha mechi mbili dhidi ya Coastal Union na Polisi Tanzania.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA MARUDIANO MISRI....MBRAZILI SIMBA NDIO KWAANZA MENO YOTE NNJE YANI...