Home Habari za michezo AHMED ALLY :- MAMBO YAMEKUWA MAGUMU KWETU…UBINGWA BASI….

AHMED ALLY :- MAMBO YAMEKUWA MAGUMU KWETU…UBINGWA BASI….

Habari za Simba SC

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahemd Ally amesema kwa walipofikia mpaka sasa kikosi hicho hakina matumanini tena ya kubeba ubingwa wa Logi Kuu Tanzania Bara kwani wamepoteza mechi wao wenyewe na kujiweka katika mazingira magumu ya kuwafukuzia wapinzani wao, Yanga Sc wanaoongoza Ligi.

Ahmed amesema hayo  Jumatano, Mei 3, 2023 wakati akizungumza na wanahabari mara baada ya mchezo wao dhidi ya Namungo ambapo Simba aliambulia sare ya bao 1-1 katika Dimba la Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.

“Hivi sasa ni kweli mambo yanadhidi kuwa magumu, tunafanya kazi ya kupunguza gape la pointi wakati huohuo tunafanya kazi ya kuongeza gape. Baada ya kumfunga kinara (Yanga Sc) kwenye mchezo uliopita tuliamini tumefanya kazi kubwa ya kupunguza gape, lakini leo tumerudi kule kule kwenye kuongeza gape.

“Kwa hiyo matumaini ya ubingwa yanazidi kufifia na tunayafifisha sisi wenyewe kwa sababu tulikuwa na hiyo nafasi ya kupunguza gape lakini leo tumeliongeza wenyewe. Kwa hiyo mambo yamekuwa magumu kwa upande wetu. Gape limekuwa alama nne na mtani akishinda gape litakuwa alama 7, kwa hiyo kwa mechi ambazo zimebaki ukweli ni kwamba tiumejiweka katika mazingira magumu kweli.

“Kwa hapa tulipofika kila mtu anaweza kuchagua upande wake, wa kukata tamaa, ana haki ya kukata tamaa wa kupambana tuendelee kupambana lakini tumejiweka kwenye hali mbaya na mambo ni magumu kweli,” amesema Ahmed Ally.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao kinara, Jean Baleke dakika ya 27, kabla ya Salum Kabunda kusawadhisha dakika ya 39 kufuatia mpira wa kona aliouokoa kipa wa Simba Ally Salum ukadondoka kwenye miguu ya Kabunda.

Simba wanaendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara wakiwa na alama 64 na michezo 27 nyuma ya Yanga wenye alama 68 na michezo 26.

Kwa matokeo hayo ya Simba, Yanga ambao kesho wataingia dimbani kukipiga na Singida BS kwenye Dimba la Liti, wanahitaji kushinda michezo miwili tu ili watangaze ubingwa wa ligi.

SOMA NA HII  KWA MIPANGO HII...SIMBA LAZIMA WAISHANGAZE AFRIKA...MASHUSHU WAANZA KAZI RASMI...