Home Habari za michezo HIVI NDIVYO MZIZE ALIVYOWAFUNIKA MASTAA WAKUBWA KWENYE LIGI…SI KAGERE WALA BOCCO….WOTE WAMEFULIA…

HIVI NDIVYO MZIZE ALIVYOWAFUNIKA MASTAA WAKUBWA KWENYE LIGI…SI KAGERE WALA BOCCO….WOTE WAMEFULIA…

Habari za Yanga SC

Tuzo ya mchezaji bora chipukizi Tanzania Bara huenda ikaenda kwa mshambuliaji kinda wa Klabu ya Yanga, Warid Clement Mzize.

Licha ya kucheza dakika chache lakini Mzize amehusika kwenye magoli (14) katika mashindano yote msimu huu.

Ligi Kuu: Mabao 5, Assis 1, dakika 533′
Kombe la Shirikisho: Mabao 6, asists 2, dakika 294′.

Mzize amehusika katika mabao mengi kuliko washambuliaji wakubwa kwenye Ligi za Tanzania mpaka sasa kwa ujumla.

❎ John Bocco
❎ Prince Dube
❎ Idriss Mbombo
❎ Collns Opare
❎ Reliants Lusajo
❎ Medie Kagere
❎ Obrey Chirwa.

Itakumbukwa kuwa Mzize ni zao la timu B ya Yanga , ambapo alianza kuaminiwa na Kocha Mkuu wa timu hiyo kwenye baadhi ya micheoz ya Ligi Kuu.

Aidha mpaka kufikia sasa, ‘kinda’ huyo ambaye amebadili dini hivi karibuni na kuwa muislamu, ni miongoni mwa wachezaji wenye idadi kubwa ya magoli kwenye Kombe la Shirikisho la Azam.

Pamoja na hayo, Mzize aliingia kwenye midomo ya mashabiki wa Yanga hivi karibuni, mara baada ya kukosa magoli ya wazi kwenye mchezo wa pili wa marudinao wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga SC na River United ya Nigeria.

Kitendo hiko kilipelekea kocha Mkuu wa Yanga, Nabi kuingilia kati na kumtetea huku akidai ni jambo la kwaida wakati mwingine mchezaji kukosa bahati ya kufunga.

Mzize atakumbukwa kuwa alianza maisha yake ya kisoka Yanga vizuri, mara baada ya kuibuka kuwa mfungaji bora kwenye ligi ya U-20 msimu uliopita huku akiisaidia Yanga B kuingia fainali ya ligi hio.

Msemaji wa Yanga , Haji Manara wakati fulani alijitokeza hadharani kumtahadharisha ‘Kinda’ huyo kukaa mbali na mambo ya starehe na wanawake, huku akidai kuwa yangeweza kumrudisha nyuma kisoka.

SOMA NA HII  DAKTARI AFICHUA KILICHOMKUMBA MWAMNYETO JUZI...ALIKUWA AHEMI TENA...