Home Habari za michezo PAMOJA NA USHINDI DHIDI YA WASAUZI JANA….NABI AIGOMEA YANGA…ATOA MSIMAMO WAKE…

PAMOJA NA USHINDI DHIDI YA WASAUZI JANA….NABI AIGOMEA YANGA…ATOA MSIMAMO WAKE…

Habari za Yanga SC

LICHA ya Yanga kushinda 2-0 nyumbani dhidi ya Marumo Gallants kwenye mechi ya kwanza nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika, kocha Mkuu wa Wanajangwani hao, Nassredine Nabi amesema hajaridhishwa na namna timu yake ilivyocheza.

Katika mechi hiyo, mabao ya Yanga yalifungwa na Stephane Aziz Ki dakika ya 63 na Benard Morrison dakika ya 90.

Akizungumza baada ya mechi kumalizika, Nabi amesema wachezaji wake hususani kipindi cha kwanza hawakucheza kama alivyowaelekeza katika uwanja wa mazoezi.

“Hatukucheza vizuri kama tulivyotaraji, tulifanya mazoezi vyema na kuiandaa mbinu tuliyoanza nayo leo lakini wachezaji walishindwa kufanya kama tulivyowafundisha na kuwaelekeza mazoezini,” alisema Nabi na kuongeza;

“Pamoja na yote tunashukuru kwa ushindi na sasa tunarudi kujipanga na mechi ya maruduano tunayoamini itakuwa ngumu ugenini ila tunahitaji matokeo yatakayotufanya kutinga fainali.”

Baada ya mechi ya jana, Yanga itarudiana na Marumo, Mei 17 mwaka huu mchezo utakaopigwa nchini Afrika Kusini.

Katika mchezo huo, Yanga inahitaji ushindi au sare ili iweze kutinga fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE