Home Habari za michezo BAADA YA YANGA KUTINGA FAINAL CAF ….SARPONG ATAMANAI KURUDI KUKIPIGA TENA …

BAADA YA YANGA KUTINGA FAINAL CAF ….SARPONG ATAMANAI KURUDI KUKIPIGA TENA …

Habari za Yanga

Nyota wa Ghana aliyewahi kukipiga katika klabu ya Yanga na Rayon Sports, Michael Sarpong ameeleza kuwa anatamani kurudi Tanzania na kuichezea ligi kuu ya Tanzania kwa mara nyingine.

Sarpong ambaye kwa sasa anaichezea Forest Rangers ya Zambia ameiambia Wasafi Media kuwa hajawahi kuisahau ligi ya Tanzania kutokana na ushindani wake mkubwa uliopo na jinsi inavyozidi kukua na kufanya vizuri kimataifa.

“Napakumbuka sana Tanzania, naipenda ligi Kuu ya Tanzania, inazidi kukua kila siku na inafanya vizuri sana kimataifa, natamani kurejea Tanzania nicheze timu yoyote ambayo naweza kuisaidia ikafanya vizuri zaidi,” amesema Sarpong.

Sarpong alisajiliwa Yanga kwa mbwembwe nyingi ambapo tofauti na matarajio ya watu  alishindwa ‘kupafomu’ na kujikuta akitupiwa lawama .

SOMA NA HII  HAWA WAPINZANI WA YANGA LIGI YA MABINGWA NAO SI HABA AISEE...WAPATA 'KOCHA LA MBINU ZA USHINDI'...ALIKUWA AL HILAL..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here