Home Habari za michezo KUHUSU MAMELOD SUNDOWNS KUMTAKA MAYELE…UKWELI WOTE HUU HAPA…YANGA HAWAWEZI KUCHOMOA HAPA…

KUHUSU MAMELOD SUNDOWNS KUMTAKA MAYELE…UKWELI WOTE HUU HAPA…YANGA HAWAWEZI KUCHOMOA HAPA…

Tetesi za Usajili Yanga

Inasemekana mabingwa wa ligi kuu nchini Afrika Kusini (PSL) Mamelodi Sundowns wameanza harakati za kuhakikisha wanainasa saini ya mshambuliaji nyota raia wa Congo DR na klabu ya Young Africans, Fiston Kalala Mayele.

FARPost inaweza kuthibitisha kwamba ripoti ya kina ya skauti iliwasilishwa kuelekea mwisho wa 2022. Hata hivyo, bado hakuna makubaliano ndani ya klabu kwa wakati ule kwamba Mayele atafaa style yao ya uchezaji hiyo, ilionekana ni vigumu kwa Sundowns kumtafuta nyota huyo wa Yanga.

Lakini mwaka huu Rulani Mokwena anaonekana kuvutiwa sana na anamhitaji Mayele kwa udi na uvumba ili akasaidiane na Peter Shalulile.

Inasemekana juzi akiwa Rustenburg wiki iliyopita kabla ya mechi ya marudiano ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Marumo, aliripotiwa kutembelewa na mwakilishi wa Sundowns.

Tayari matajiri hao wa Kusini mwa Afrika almaarufu kama “Masandawana” wameshatenga fungu la kutosha kwa ajili ya mshambuliaji huyo kinara wa mabao kwenye ligi kuu nchini Tanzania pamoja na kombe la shirikisho Afrika.

Kwa ubora ambao Fiston Mayele ameuonyesha tangu atue nchini ni lazima aingie kwenye matamanio ya vigogo wengi sana wa soka hapa barani Afrika.

SOMA NA HII  AMRI KIEMBA AFUNGUKA YA MAYONI BAADA YA KUIONA SIMBA IKIKOSA HUDUMA ZA CHAMA NA LUIS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here