Home epl IHEANACHO AENDELEA KUWABEBA LEICESTER

IHEANACHO AENDELEA KUWABEBA LEICESTER

 


KELECHI Iheanacho amewasogeza karibu zaidi Leicester City kwenye mbio za kumaliza kwenye nne bora katika Ligi Kuu England baada ya kuwapa ushindi juzi.

 

Leicester City walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace kwenye mchezo muhimu kwao.

 

Mshambuliaji huyo ambaye amekuwa kwenye kiwango cha juu msimu huu alifanikiwa kufunga bao la pili kwa ufundi wa hali ya juu.Sasa Leicester wamefikisha pointi 59 zikiwa ni saba mbele ya West Ham waliopo nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.

 

Hata hivyo, kwenda juu nafasi ya pili ni kazi ngumu kwao kwa kuwa pia wapo nyuma ya Man United kwa tofauti ya pointi saba.Iheanacho amekuwa mchezaji muhimu kwenye timu hiyo akiwa amefanikiwa kufunga mabao 14 katika michezo 14 ya michuano yote iliyopita

SOMA NA HII  AL AHLY WAENDELEZA UBABE AFRIKA...WATINGA NUSU FAINALI KLABU BINGWA KWA KISHINDO...