Home Habari za michezo BAADA YA KUWATAZAMA YANGA…KOCHA WA USM ALGER KANUGA WEE..KISHA AKASEMA HAYA…

BAADA YA KUWATAZAMA YANGA…KOCHA WA USM ALGER KANUGA WEE..KISHA AKASEMA HAYA…

Habari za Yanga

Kocha Mkuu wa USM Alger ya Algeria, Abdelhak Benchikha amesema hana hofu na kiwango cha Yanga na wategemee mechi ngumu zaidi ya zote zilizopita kwani wanahitaji kombe hili.

“Wanatakiwa kufahamu kuwa wanakwenda kukutana na timu ya tofauti kuliko walizokutana nazo katika hatua waliyocheza,tunalihitaji hili kombe,tunaheshimu uwezo wao,” Kocha USM ALGER, Abdelhak Benchikha.

Yanga atakutana na USM, Jumapili ijayo, Mei 28, 2023 katika mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa katika Dimba la Mkapa jijini dar es Salaam na mchezo wa pili utapigwa Algeria Juni 4.

USM ALger imetinga fainali ya michuano hiyo kwa kuiondoa AS FAR Rabat ya Morocco kwa jumla ya mabao 4-3 huku Yanga ikiiondoa Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 4-1.

SOMA NA HII  A-Z JINSI YANGA NA SIMBA ZILIVYOPAPATUANA BILA KUTOBOANA JANA...YANGA YAENDELEZA UBABE....