Home Habari za michezo “SIMBA TUMEPIGWA NA TAHARUKI FEDHA WANAZOTAKA WACHEZAJI…AHMED ALLY AFUNGUKA A-Z

“SIMBA TUMEPIGWA NA TAHARUKI FEDHA WANAZOTAKA WACHEZAJI…AHMED ALLY AFUNGUKA A-Z

SIMBA TUMEPIGWA NA TAHARUKI FEDHA WANAZOTAKA WACHEZAJI...AHMED ALLY AFUNGUKA A-Z

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa wamepigwa na taharuki baada ya kusikia fedha wanazohitaji wachezaji wao kipindi cha usajili.

Ahmed amesema kuwa gharama za kuendesha Klabu zimepanda sana na kama ni kweli Wachezaji wanataka fedha hizo basi hakuna klabu Tanzania yenye uwezo wa kuzalisha nyingi hivyo kutoka kwenye vyanzo vyake bali tunamtegemea Muwekezaji.

Ameongeza kuwa ni kawaida ya Binadamu haoni umuhimu wa neema aliyokua nayo mpaka iondoke.

Amewataka wana Simba kumtetea na kumlinda Mohamed Dewji juu ya wale wote ambao wanamuona hafai wakati ndiye aliyeifikisha Simba hapa ilipo.

Hii ni baada ya mwanachama wa Simba na Mbunge wa Makete, Festo Richard Sanga kuchapisha andiko akimtaka Mo Dewji aiachie Simba ili watu wengine waje kuwekeza.

Aidha, Ahmed amesema hiki ndicho kipindi ambacho Simba inamuhitaji zaidi Mohamed Dewji kuliko kipindi chochote na kufanya vibaya kwa Simba kwa misimu miwili mitatu isiwe sababu ya kufuta yote mazuri yaliyofanyika.

“Ni fedha za Mo Dewji ndio zimeitoa Simba mavumbini na kuifikisha nafasi ya 7 Afrika. Ni Fedha za Mo Dewji zimetupa Ubingwa mara nne mfululizo Ni Fedha za Mo Dewji zimetupa robo Fainali tano za CAF mfululizo.

“Fedha za Mo ndizo zimetuweka kwenye ramani ya soka la Afrika na tunatajwa kuwa timu kubwa katika bara hili. Kufanya vibaya misimu hii ndio ionekane Mo hafai?? Tumtolee mapovu na kumvunjia heshima? Unadhani kupata Mwekezaji kwenye mpira ni rahisi?

“Tuache kudanganyana eti kuna Mwekezaji anaitaka Simba kwa Bilioni 40, alikua wapi wakati Simba tunanyanyasika na Utawala wa Yusuph Manji, alikua wapi wakati mchakato wa Tender uko wazi.

“Ndugu zangu wana Simba tusingie kwenye huu mtego tutakuja kulia kilio cha Punda pale Mo atakapo amua vinginevyo. Lipo kundi la watu wamepandikizwa kumkatisha tamaa Mo aondoke ili Simba turudi kwenye msoto.

“Kuwekeza kwenye football sio swala la fedha tu ni swala la Passion, England pamoja na kuwa na Matajiri wengi lakini Wawekezaji wengi wa vilabu wanatoka nje ya nchi hiyo.

“Hivyo tusijidanganye kuwa Tanzania kuna Matajiri wengi watawekeza tuu Ni Jukumu letu Wana Simba kumlinda Mo, Kumtetea Mo, na kumpigania kwa maslahi ya Simba yetu.

“Kufanya vibaya kwa timu ni jambo la kawaida, Chelsea ni miongoni mwa timu zenye Wawekezaji Matajiri lakini wanasota kwenye EPL. Hivyo sisi kufanya vibaya kwa misimu hi tusimtoe maana Muwekezaji wetu bali tumtie moyo ili afanye zaidi.

“Tuwe makini na Mamluki wanaoneza chuki dhidi ya Mwekezaji wetu, Ukweli tuu kwamba tunamuhitaji sana Mo kipindi hiki kuliko kipindi chochote. Gharama za Mpira zimepanda sana, Wote tumepigwa na taharuki baada ya kusikia fedha wanazohitaji Wachezaji wetu kipindi cha usajili.

“Kama ni kweli Wachezaji wanataka fedha hizo basi hakuna klabu Tanzania yenye uwezo wa kuzalisha nyingi hivyo kutoka kwenye vyanzo vyake bali tunamtegemea Muwekezaji. Kawaida ya Binadamu haoni umuhimu wa neema aliyokua nayo mpaka iondoke. Tajiri apepewe.”

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA WAIVORY...MO DEWJI AKUNJUA POCHI SIMBA....ATOA AHADI YA MAMILIONI..BOCCO AJIFUNGA ULIMI..