Home Habari za michezo MASHUSHU WA CAF WAVAMIA HOTEL YA YANGA…WATOA ‘DATA’ ZA WASAZUI NA TAHADHARI…

MASHUSHU WA CAF WAVAMIA HOTEL YA YANGA…WATOA ‘DATA’ ZA WASAZUI NA TAHADHARI…

Habari za Yanga SC

Wakati wachezaji wa Yanga wakimalizia kula chakula cha mchana katika hoteli waliyofikia hapa Rustenburg, Afrika Kusini na viongozi wengine wakiendelea na shughuli za kitimu, ghafla waliingia Maofisa wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), ambao hawakutoa taarifa kabla.

Viongozi hao walikuwa watatu mmoja akiwa amevalia fulana yenye nembo ya CAF na wengine nguo za kawaida na kuingia moja kwa moja hotelini.

Walipoingia mlangoni walikutana na Meneja wa Yanga, Walter Harrison na ofisa wa ulinzi wa timu hiyo maarufu Penta na kuanza kuzungumza.

Mazungumzo ya viongozi hao wa CAF na wale wa Yanga yalidumu kwa muda usiozidi dakika 10 kisha kuondoka.

Inaelezwa viongozi hao walifika kambini hapo kuangalia usalama wa timu na kutoa baadhi ya maelekezo kuhusu mambo yanayohusu mchezo wa Marumo Gallants na Yanga.

Ikumbukwe leo saa 1:00 usiku za Tanzania na 12:00 jioni za hapa Afrika Kusini, Marumo wataikaribisha Yanga uwanjani kwenye mchezo wa pili nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga inahitaji ushindi au sare ya aina yeyote kwenye mechi hiyo ili kutinga fainali kwani ilishinda 2-0, nyumbani Tanzania kwenye mechi ya duru ya kwanza.

SOMA NA HII  WAKATI JAHAZI LA MAN UTD LIKIWA HALIELEWEKI...RIO FERDINAND ATABIRI HAYA KUHUSU RONALDO...