Home Habari za michezo MAGAZETI SAUZI YAUZA NA STORI ZA YANGA TU….TIMU WENYEJI WAPEWA ‘ODDS’ NDOGO…

MAGAZETI SAUZI YAUZA NA STORI ZA YANGA TU….TIMU WENYEJI WAPEWA ‘ODDS’ NDOGO…

Habari za Yanga SC

Baadhi ya magazeti ya hapa Afrika Kusini kwenye kurasa za michezo yameandika kuhusu Yanga kushinda ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC siku chache kabla ya mechi ya marudiano dhidi ya Marumo Gallants hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Tofauti ya timu hizi mbili [Yanga na Marumo Gallants] ipo hivi, Marumo Gallants inapigana kujinusuru isishuke daraja kwenye Ligi yake wakati Yanga yenyewe tayari bingwa kwenye Ligi ya Tanzania!

Kwa hiyo baadhi ya magazeti yamejaribu kuangalia tofauti ya timu hizi kwa upande wa Ligi zinazoshiriki na umuhimu wa mchezo kati yao.

Yanga ina mechi mbili za Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons huku tayari ikiwa bingwa lakini Marumo yenyewe ina mchezo mmoja dhidi ya Swallows wa Ligi ya Afrika Kusini ambao utaamua hatma yao ya kubaki Ligi Kuu au kushuka daraja.

SOMA NA HII  ROBERTINHO HANA WASI NA ZAMBIA, AWATUMIA WAMBA HAWA KUMALIZA KAZI