Home Uncategorized NYOTA WA STARS ANASHINDA NDANI NCHINI MISRI KISA KORONA

NYOTA WA STARS ANASHINDA NDANI NCHINI MISRI KISA KORONA


HIMID Mao, nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania anayekipiga soka la kulipwa nchini Misri kwenye Klabu ya ENPPI amesema kuwa kwa sasa wao wanashinda ndani ili kukepwa maambukizi ya Virusi vya Corona.

Kiungo huyo abaye ni nahodha msaidizi wa Taifa Stars amesema kuwa kutokana na maambukizi ya Corona shughuli nyingi zimesisimama jambo linalowafanya waendelee kuwa ndani.

“Kwa sasa shughuli nyingi zimesimama ikiwa ni pamoja na ishu ya masuala ya soka hivyo kabla ya ligi kusimamishwa tulipaswa kucheza mchezo mmoja ulighairishwa kutokana na mvua lakini baadaye tukaambiwa kwamba ligi itasimama kutokana na maambukizi ya Corona.

“Nipo salama na ninaendelea vizuri hicho ninashukuru kwa Mungu,” amesema

SOMA NA HII  MBWANA SAMATTA NA ASTON VILLA YAKE MAJANGA MATUPU HUKO ULAYA