Home Uncategorized HOFU YA WACHEZAJI KUPATA MAJERAHA YAONGEZEKA IWAPO LIGI YA ENGLAND ITAMALIZIKA JUNE...

HOFU YA WACHEZAJI KUPATA MAJERAHA YAONGEZEKA IWAPO LIGI YA ENGLAND ITAMALIZIKA JUNE 30


MADAKTARI wa timu zinazoshiriki Ligi Kuu England wamewaonya mabosi wa timu zinazoshiriki Ligi Kuu England kwamba wanapaswa wajiandae na kesi za wachezaji wao kuumia misuli iwapo watajaribu kumaliza ligi hiyo June 30.



Kwa sasa mechi za Ligi Kuu England zimesimama kupisha maambukizi zaidi ya Virusi vya Corona na inatarajiwa kurejea kuanza mwezi Aprili 30 huku ikitarajiwa kukamilika June 30.

Wasiwasi wa uwepo wa Virusi hivyo unafanya ligi kufikiriwa kuwa iwapo itaanza kuchezwa Mei Mosi kutakuwa na mechi nyingi kwa timu moja jambo ambalo lina hatari kwa afya za wachezaji.

Kutokana na kesi hii hakuna timu yenye njia mbadala zaidi ya kukubaliana na hali na itawalizimu kucheza mechi mbili ama tatu ndani ya wiki moja ili kukimbizana na muda huku zile zinazoshiriki michuano ya Kombe la FA watakuwa na ratiba ngumu ambazo za kukamilisha.

Mmoja wa madakatari wa timu ambazo zipo nafasi ya juu amesema kuwa ni agizo kubwa kwa wachezaji kucheza Jumamosi, Jumatano na Jumamosi tena ni ratiba iliyobana na itakusanya majeruhi wengi bila mashaka.

SOMA NA HII  MBARAZIL WA SIMBA AKIWASHA HUKO SAUZI