Home Habari za michezo HUU HAPA MKAKATI WA BILIONEA WA YANGA KUHUSU NDOO YA AFRIKA…KAZI INAANZA...

HUU HAPA MKAKATI WA BILIONEA WA YANGA KUHUSU NDOO YA AFRIKA…KAZI INAANZA LEO RASMI…

Habari za Yanga SC

Baada ya Yanga kuibuka na ushindi wa maboa 2-0 dhidi ya Marumo Gallants na kuweka mguu mmoja ndani ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, Bilionea wa Yanga, Ghalib Said Mohammed ‘GSM’, amesisitiza kuwa anataka kuona kikosi hicho kikishinda ubingwa wa mashindano hayo.

GSM ambaye Jumatano iliyopita alihudhuria uwanjani pamoja na familia yake na kushuhudia Yanga wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo aa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Yanga ambao ni wawakilishi pekee wa Tanzania waliosalia kwenye mashindano ya Kimataifa sasa wanajiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Marumo, mchezo ambao unatarajiwa kupigwa Afrika Kusini leo Jumatano  ambapo Yanga wanahitaji angalau matokeo ya sare yoyote ili kutinga hatua ya fainali.

Akizungumza nasi, GSM alisema: “Tunashukuru kwa kufanikiwa kupata ushindi katika mchezo huu, hii ni hatua kubwa kwetu lakini tunafahamu bado kuna kazi kubwa ya kufanya kwenye mchezo wa marudiano ugenini ambao ni wazi utakuwa mchezo mgumu.

“Tunajiandaa na tunataka kupata matokeo mazuri kwenye mchezo huo ili kutimiza malengo ya kushinda ubingwa wa mashindano haya, tunajua sio rahisi lakini tupambana kufanikisha hilo.”

SOMA NA HII  YANGA SC YATOA WAWILI KIKOSI BORA SHIRIKISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here