Home Uncategorized YANGA: MBINU ZA EYMAEL ZIMEJIBU, MASHABIKI WANASTAHILI PONGEZI

YANGA: MBINU ZA EYMAEL ZIMEJIBU, MASHABIKI WANASTAHILI PONGEZI


JUMA Abdul, nahodha msaidizi wa Yanga amesema kuwa kazi ndo inaanza kwa Yanga baada ya mbinu za Kocha Mkuu, Luc Eymael kujibu kwa sasa pamoja na sapoti ya mashabiki.

Beki huyo wa Yanga amekuwa kwenye uimara wake baada ya kurejea uwanjani msimu huu ametoa jumla ya pasi tatu za mabao akiwa ni beki mwenye pasi nyingi ndani ya Yanga.

Akizungumza na Saleh Jembe, Abdul amesema kuwa Eymael amewapa mbinu nyingi ngumu zinazowapa matokeo mazuri.

“Kwa sasa tumeanza kurejea kwenye ubora wetu taratibu japo haijawa kwa kasi kubwa ila tunajua kile ambacho tunakitaka pamoja na mashabiki wanachokitaka, mbinu za kocha zinatupa matokeo mazuri na tayari zimeanza kujibu.

“Ushindani ni mkubwa na kila timu inapambana kutafuta matokeo chanya, tunaomba Mungu tuendelee kuwa na matokeo bora ili tufikie malengo yetu, mashabiki pia wamekuwa wakitupa sapoti tunawashukuru katika hili wasichoke” amesema Abdul.

Yanga ipo nafasi ya tatu ikiwa imecheza mechi 18 na ina pointi 37 kibindoni. 
SOMA NA HII  VIDEO:PENALTI ZA MARCO MZUMBE NA SAID KATUNDU JR ZAWAPA USHINDI WASIOOA