Home Uncategorized AZAM FC YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA POLISI TANZANIA

AZAM FC YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA POLISI TANZANIA


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa wanahitaji pointi tatu za Polisi Tanzania kwenye mchezo utakaochezwa Jumanne, Februari 11,2020, Uwanja wa Uhuru.

Azam FC jana imeshinda mabao 3-1 mbele ya KMC inafikisha jumla ya pointi 41 ikiwa nafasi ya pili.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga, amesema kuwa kila kitu kipo sawa wataendelea kupambana.

“Tunashukuru kwa kushinda mbele ya KMC, tunahitaji ushindi mbele ya Polisi Tanzania ili kuendelea mwendo wetu wetu wa kufukuzia malengo yetu ambayo tumejiwekea,” amesema. 

SOMA NA HII  NYOTA HAWA WATATU KIKOSI CHA KWANZA SIMBA WAMSHANGAZA MBELEGIJI