Home Habari za michezo ILE ISHU YA SAOTHAMPTON YA UINGEREZA KUTAKA KUMSAJILI MTZ NOVATUS IKO HIVI….

ILE ISHU YA SAOTHAMPTON YA UINGEREZA KUTAKA KUMSAJILI MTZ NOVATUS IKO HIVI….

Tetesi za Usajili

Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Mail, Timu ya Southampton na Middlesbrough wameonesha nia ya kumsajili Novatus Dismas Miroshi kutoka klabu ya Zulte Waregem ya Ubelgiji.

Novatus mwenye umri wa miaka 20 alijiunga na Zulte msimu uliopita kutoka nchini Israeli, lakini ameendelea kuvutia kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi nyingi uwanjani.

Msimu huu Novatus amecheza kama kiungo, beki wa kushoto na wakati mwingine beki wa kati kwenye mfumo wa back three.

Licha ya timu yake kushuka daraja bado Miroshi ameendelea kuvivutia vilabu vikubwa.

Msimu huu Novatus amecheza michezo 36 akiwa na Zulte Waregem na kutoa pasi mbili za magoli huku akiichezea Taifa Stars na kufunga mabao mawili.

SOMA NA HII  KIUNGO HUYU MZAMBIA KUTUA SIMBA